ANTONIO CONTE AVIJIA JUU VYOMBO CHA HABARI - Darajani 1905

ANTONIO CONTE AVIJIA JUU VYOMBO CHA HABARI

Share This
Kama ilivyo kwaida ya kocha Antonio Conte kuongea au kufanya mkutano na waandishi wa habari kila tu inapobaki siku moja ili timu yake ishuke uwanjani, leo kuelekea kwenye mchezo huo wa kesho dhidi ya Leicester city ambapo Chelsea itakuwa nyumbani amefanya mahojiano hayo, a hapa aikuwa akizungumzia mustakabali wake klabun hapo mara baada ya kuwepo tetesi za kuachana na Chelsea ufikapo mwisho wa msimu.

"Nina mwaka mwengine katika mkataba wangu wa kuwa mahali hapa lakini kwenye soka jambo lolote linaweza kutokea. Toka msimu umeanza mmekuwa mkirirudia sana hili swali. Nawaruhusu mnifukuze ila kila siku huwa nawaambia kwa kocha yoyote wa klabu kama hii ni kawaida kufukuzwa pale timu inapokuwa katika hali hii"

"Hii ndio historia ya klabu hii. Nami naweza kupambana na hali kama hii, lakini kuna jambo linanishangaza toka tulipopoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Burnley, vyombo vya habari vimekuwa vinataka nitoke na nafasi yangu ichukuliwe na mtu mwengine. Kwa klabu nyengine hili halitokei kwao. Najiamini kwa kile nachokifanya na vile timu yangu ilivyo mpaka sasa tunatimiza msimu wa pili. Lakini kwenye soka jambo lolote linaweza kutokea inatakiwa tuwe tayari kwa lolote"

"Zamani makocha walikuwa wapo kwenye timu kwa miaka mingi. Lakini kwa sasa haswa hapa Uingereza kumekuwa na tabia hii ya kufukuza makocha mapema. Sintoshangaa kwa maana lolote linaweza kutokea. Historia ya Chelsea inajieleza. Ni kawaida kwa waandishi wa habari ukiwa kwenye mkutano wakakuuliza mengi kuhusiana na kibarua chako. Lakini hali ndio ipo hivyo, haiwezi kubadilika"

"Nina furaha na napendezwa kuwa mahali hapa kwa kipindi chote hiki, haikuwa rahisi haswa kwangu kwa kufanya kazi nje ya nchi kwa mara ya kwanza. Nafurahia kuwa Uingereza na hata hali yake ya mazingira naipenda" alisema kocha huyo Antonio Conte

Lakini ni inaweza kuwa kweli kwamba kocha Antonio Conte hana mpango wa kuondoka klabuni na hata anaonekana kuwa na furaha mara zote kuwa Chelsea ila vyombo vya habari mara nyingi vimekuwa ni kama havitaki aendelee kubaki Uingereza, na kama utakuwa una kumbukumbu nzuri msomaji wangu toka mwanzo wa msimu wachambuzi wengi na mitandao mingi ilikuwa ikimtabiria kufanya vibaya msimu huu na hata kumtaja kuwa kocha wa kwanza kuondoka klabuni Chelsea.

Lakini pia moja ya magazeti maarufu barani Ulaya liliwai kuripoti, mara baada ya mchezo wa Chelsea dhidi ya Manyumbu(Man utd) kuwa kuewepo nje kwa nyota David Luiz ni kwa kuwa nyota huyo alikuwa mpatanishi katika ugomvi au kutokuelewana kwa kocha Conte na nyota wa zamani wa Chelsea, David Luiz lakini hakukuwa na kuonyesha kuwa kweli Luiz aliongea mwenyewe na kuhisi hivyo.

No comments:

Post a Comment