Mara ya baada kuonyesha kiwango bora katika mchezo wa robo fainali ya kombe la ligi Carabao Cup, nyota Ethan Ampadu ametoa siri kwamba wakati akiwa mdogo alishawai kuwa shabiki wa Chelsea.
Ampadu alisema "nimekuwa shabiki wa Chelsea toka nikiwa mdogo, nilikuwa na ndoto za kucheza hapa. Nilikuwa namwangalia na kumfurahia sana Didier Drogba na jinsi anavyocheza licha sichezi nafasi aliyokuwa anacheza. Lakini kuwatazama nyota ambao najifunza kutoka kwao, najifunza haswa kwa John Terry na Gary Cahill" alisema na kumalizia kiungo mkabaji huyo ambaye kocha wa timu yake ya taifa ya Wales aliwai kumsifia na kukiri kuwa Ampadu ana uwezo wa kucheza nafasi nne mpaka tano uwanjani.
Hongera nyota wetu Ethan Ampadu.
No comments:
Post a Comment