N'Golo Kante aanza mazungumzo ya kuachana na Chelsea - Darajani 1905

N'Golo Kante aanza mazungumzo ya kuachana na Chelsea

Share This

Moja ya viongozi wa klabu ya PSG ambaye anashughulika na mambo ya usajili klabuni hapo anatajwa kufanya mazungumzo na wawakilishi wa nyota wa Chelsea, N'Golo Kante ili ajiunge na klabu yao mabingwa wa ligi kuu nchini Ufaransa maarufu kama Ligue 1.

PSG wanatajwa kumfanya Kante kama chaguo lake la kwanza katika usajili wakiwa na lengo la kukiimarisha kikosi chake katika nafasi ya kiungo haswa kutokana na kiungo wake mwenye madaraka ya kiungo mkabaji (defensive midfilder), Thiaggo Motta kukaribia kuachana na klabu hiyo kutokana na umri wake kumtupa mkono.

Chelsea iliyomsajili Kante kutokea klabu ya Leicester city mwaka 2016 inatajwa kutotaka kumpoteza nyota huyo ambaye msimu huu amefanikiwa kushinda tunzo mbili klabuni hapo akishinda tunzo ya mchezaji bora wa mwaka pamoja na tunzo ya mchezaji bora klabuni hapo akizawadiwa na mdhamini mkuu klabuni hapo, kampuni ya Yokohama Tyres.

No comments:

Post a Comment