CONTE AMTETEA CHRISTENSEN, ASEMA NI MCHEZAJI BORA - Darajani 1905

CONTE AMTETEA CHRISTENSEN, ASEMA NI MCHEZAJI BORA

Share This
Chelsea ilicheza soka safi huku wakitumia zaidi mashambulizi ya kushtukiza katika mchezo wa jana ambao uliisha kwa suluhu ya magoli 1-1 dhidi ya wababe wa Hispania, Barcelona ambapo walipata goli lao mara baada ya walinzi wa Chelsea kutokuwa na kutokuelewana ambapo Christensen alitoa pasi katika eneo la nyuma ambapo pasi yake haikumlenga mtu anayempasia na hivyo kuambaambaa kabla ya kiungo wa Barcelona, Andes Iniesta kuunasa na kumpasia Messi aliyefunga goli jepesi kabisa.

Mara baada ya kosa hilo kufanyika, kocha Antonio Conte, alieleza "Alikuwa na uwezo mkubwa sana. Tunamuongelea mchezaji ambaye umri wake ni mdogo sana, ni jambo la kushangaza hata kwa kuweza kwake kucheza mchezo wa huu huku akionyesha ukomavu wa hali ya juu na uwezo mkubwa. Alikuwa mmoja ya waliocheza soka safi"

"Ni ngumu kumuelezea mchezaji mmoja lakini naamini Christensen alicheza soka la kiwango cha juu na nilikuwa nna uhakika na kiwango chake. Tulifanya kosa moja lakini najua kucheza na wapinzani kama Iniesta, Messi na (Luis) Suareza, ukifanya kosa basi ni lazima likugharimu" alisema Conte.

Klabu hizo zitarudiana katika mchezo wa pili ambapo Chelsea itasafiri kwenda nyumbani kwa Barcelona, Camp Nou ambapo huko itahitaji kupata ushindi wowote au suluhu ya magoli ya kuanzia 2-2 na kuendelea ili kufanikiwa kufudhu na sio kupata sukuhu ya 0-0 ambapo itamaanisha hatutofanikiwa kufudhu. Na kama mchezo ukiisha kwa suluhu ya 1-1 basi zitaongezwa dakika 30 na baadae ngoma ikiwa ngumu maana yake mchezo utaamuliwa kwenye matuta.

No comments:

Post a Comment