UEFA; MORATA, GIROUD WOTE NJE-CHELSEA vs BARCELONA - Darajani 1905

UEFA; MORATA, GIROUD WOTE NJE-CHELSEA vs BARCELONA

Share This
Chelsea inashuka uwanjani usiku huu kupambana dhidi ya Barcelona katika mchezo wa raundi ya 16 bora ya klabu bingwa Ulaya ambapo ni mchezo wa kwanza kuchezwa kabla ya tarehe 14-Marchi kuchezwa mchezo wa pili baina ya timu izo na mshindi wa jumla ndie atakayefudhu kucheza hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.
Hapa nakuletea kikosi cha Chelsea kitakachoingia uwanjani kupambana katika mchezo huo;

Kipa; Thibaut Courtois
Walinzi; Cesar Azpilicueta (C) | Andreas Christensen | Antonio Rudiger
Viungo; Moses | Kante | Fabregas | M.Alonso
Washambuliaji; Willian B. | Eden Hazard | Pedro R.
Wachezaji wa akiba; Willy Caballero, Gary Cahill, Zappacosta, Hudson-Odoi, Drinkwater, Giroud na Morata

Kwa kikosi hichi, kocha Antonio Conte anaonekana kutaka kuwatumia washambuliaji wenye kasi watakaotumika zaidi kwenye mashambulizi ya kushtukiza na kuitusua ngome ya Barcelona. Anamtumia Eden Hazard kama mshambuliaji wa kati wakati kuna Alvaro Morata na Olivier Giroud ambao wote kiasili ni washambuliaji wa kati lakini ameamua kumtumia Hazard kwa nafasi hiyo ambaye kiasili sio mshambuliaji wa kati kutokana na kasi yake.

No comments:

Post a Comment