UEFA; WILLIAN NI HATARI-CHELSEA 1-1 BARCELONA - Darajani 1905

UEFA; WILLIAN NI HATARI-CHELSEA 1-1 BARCELONA

Share This
Hatimaye kabumbu kubwa limechezwa huko kwenye uwanja wa Stamford Bridge, uwanja unaopatikana kwenye jiji la London kwa upande wa magharibi.
Mchezo huo umeisha kwa sare ya mabao 1-1 huku nyota wa Chelsea, Willian akigongesha miamba mara mbili mfululizo katika kipindi cha kwanza. Ambapo katika kipindi hicho, matokeo yalikuwa 0-0, huku klabu hizo zikigawana, yaani Chelsea ikitengeneza nafasi nyingi za magoli, nafasi 6 huku nafasi 3 zikiwa zimelenga lango. Wakati kwa upande wa Barcelona, wao walimiliki mpira na kuuchezea kwa muda mrefu ambapo mpaka kipindi cha kwanza kinaisha, Barcelona walikuwa na umiliki wa mpira 71% wakati kwa upande wa Chelsea ikimiliki kwa 29%.

Kipindi cha pili dakika ya 62 ndiyo ilikuwa dakika iliyoamsha shangwe za mashabiki wengi wa Chelsea, mara baada ya winga wake raia wa Brazil, Willian Borges akifunga kwa shuti la nje ya eneo la hatari.

Lakini dakika 13 baadae, yaani dakika ya 75, Lionel Messi akaifungia Barcelona goli la kusawazisha ambalo pia lilimaanisha Barcelona kupata goli la ugenini.
Mpaka mpira unaisha, Chelsea 1-1 Barcelona.

Kwa matokeo haya, Chelsea inahitaji kupata ushindi au suluhu ya magoli zaidi ya mawili ili kuweza kufudhu kucheza hatua ya robo fainali ambapo mchezo wa marudiano utakuwa tarehe 14-Marchi.

No comments:

Post a Comment