Ukurasa huu una vipengele vikuu vitano, ambavyo ni Chelsea Habari, Chelsea Usajili, Chelsea HD, Mitandaoni pamoja na Majirani.
- Chelsea Habari; hiki ni kipengele maalumu kwa ajili ya kukuletea habari zote zinazoihusu klabu ya Chelsea pamoja na vilabu vilivyochini ya klabu hiyo ambavyo ni klabu za Vijana wa akademi (Chelsea Youth) pamoja na klabu maalumu kwa soka la akina dada (Chelsea Ladies) lakini pia habari za klabu yenyewe ya wanaume (Chelsea FC)
- Chelsea Usajili; hiki ni kipengele kinachokuletea habari zote kuhusu tetesi za usajili na hata sajili zilizokamilika kwa wachezaji walionunuliwa ama kuuzwa na Chelsea au hata wanaotajwa kutoka ama kuingia ndani ya klabu hizo.
- Chelsea HD; hiki ni kipengele maalumu kwa ajili ya kukuletea matukio yote yaliyotokea klabuni Chelsea
- Mitandaoni; kipengele hiki ni maalumu kwa ajili ya kukuletea matukio yote yanayoihusu klabu ya Chelsea na watu wake klabuni hapo katika mitandao ya kijamii.
- Majirani; kipengele hiki ni maalumu kwa kukuletea habari za wachezaji waliopo kwa mkopo kwenye vilabu vyengine wakitokea Chelsea, lakini pia wakongwe na wachezaji wote waliowai kuichezea au kuitumikia klabu ya Chelsea.