Chelsea ilikuwa tayari kutoa dau la euro milioni 58 ili kumnasa mlinzi raia wa Senegal anayeichezea klabu ya Napoli, Kalidou Koulibaly katika dirisha kubwa la usajili lililopita, lakini nyota huyo hakukamilisha usajili wake wa kutua klabuni Chelsea.
Lakini sasa Chelsea inatajwa kurudi tena kwa nyota huyo mwenye miaka 26 kwa sasa huku akitajwa kati ya walinzi bora kwa miaka minne aliyocheza kwenye ligi hiyo ya nchini Italia maarufu kama Serie A huku dau linalotajwa kuweza kumng'oa nyota huyo kwenye klabu hiyo likiwa ni paundi milioni 60.
Lakini pia Chelsea inatajwa kuingia kwenye mbio za kumsajili mlinzi huyo kwa sharti moja tu, kama kocha Antonio Conte ataendelea kubaki klabuni Chelsea basi ndio itamaanisha kusajiliwa kwa nyota huyo maana inaelezwa kuwa kocha huyo ndiye anashawishi kusajiliwa kwa mlinzi huyo mwenye uwezo mkubwa wa kucheza kama mlinzi wa kati.
No comments:
Post a Comment