CHELSEA HAINA UWANJA? UFAFANUZI HUU HAPA - Darajani 1905

CHELSEA HAINA UWANJA? UFAFANUZI HUU HAPA

Share This
Kumekuwa na hadithi na stori nyingi zimekuwa zikiendelea juu ya umiliki wa uwanja wa Chelsea maarufu kama Stamford Bridge, wengi wamekuwa wakipata kejeli na hata kusemwa vibaya haswa mashabiki wa Chelsea kuwa klabu yetu haina uwanja na ule tunaoutumia ni uwanja wa serikali.

Sasa hapa nakuletea majibu kamili kuhusu kejeli hizo na hadithi hizo ambazo zimekuwa zikivumishwa na mashabiki wa klabu mbalimbali juu ya klabu yetu pendwa ya Chelsea.

Uwanja wa Stamford Bridge ulijengwa na kuanza kutumika mwaka 1877 (ukitumika zaidi kama uwanja wa riadha na mikutano inayofanana na riadha).
Miaka 29 baadae (1904), ulinunuliwa (pamoja na maeneo mengine yaliyozunguka) na mfanyabiashara Gus Mears kuugeuza kwa ajili ya soka.
Mears  alijaribu kuuza eneo hilo kwa klabu ya Fulham, ambayo haikuwa na uwezo wa kuinunua...ndipo Mears alipoamua kuanzisha timu yake, ili itumie uwanja huo. Kinyume na timu nyingine ambazo huanzishwa kisha kutafuta uwanja baadae, Chelsea ilianzishwa (1905) na kina Mears tayari kukiwa na uwanja wa kuchezea. Uwanja huo hadi sasa unajulikana kama Stamford Bridge.
Kina Mears waliendelea kumiliki uwanja na timu hadi miaka ya 1970, walipoamua kuuboresha zaidi uwanja ili uweze kukaliwa na watazamaji 50,000. Baadhi ya marekebisho yalianza kufanyika, ila kufikia miaka ya 1975, upanuzi ulianza kulega kutokana na hali ya kifedha ya kina Mears na ndipo wamiliki wakaamua *kutenganisha timu na uwanja* kuwa vitega uchumi vinavyojitegemea.
Kufikia mwishoni mwa miaka ya sabini, kina Mears waliamua kuuza timu na kuuza uwanja (kila kimoja tofauti na kingine). Kwa kuwa timu ndiyo ilikuwa inajenga uwanja na ilikuwa na madeni mengi, Bwana Ken Bates alinunua *klabu* kwa bei ya kutupa ya £1 mwaka 1982.
Matajiri wengine wa real estate (Marler Estates), nao wakanunua uwanja separately.
Bwana Bates akawa na mapambano mengi ya kisheria kati yake na Marler Estates, ambayo yalidumu hadi 1990 ambapo mtikisiko wa real estate ulipopelekea Marler Estates kufilisika.
Bates akaweza kununua tena uwanja na kuunganisha tena na klabu kuwa kitu kimoja.
Kufikia 1996, Bates akaipeleka Chelsea Village (kumbuka ile holding company ambayo baadaye itakuja kubadilishwa na Abramovich kuwa Chelsea FC PLC) kwenye soko la hisa (AIM Stock Exchange).
Kufuatia hilo la kwenda sikoni, wapenzi wa Chelsea wakajiunda na kutengeneza kampuni (public company lakini isiyojiendesha kwa faida), inayoitwa CPO (Chelsea Pitch Owners), ambao walinunua hisa kwenye Chelsea Village PLC, kwa nia ya kuhakiksha klabu yao haifiki hali ya kufilisika kutakapopelekea kuuzwa kwa kiwanja chao tena (kama kina Mears walivyofanya kwa Marler Estate).
Timu ya baadhi ya wamiliki au wanachama wa CPO walipojiunga na kuingia kwenye mashindano yao binafsi hii ilikuwa mwaka 2016
CPO ikanunua haki zote za uwanja, pamoja na jina la timu (Chelsea FC) kupitia mkopo wa £10m walioupata kutoka Chelsea Village PLC.
CPO wakaukodisha uwanja wa Stamford Bridge kwa timu ya Chelsea FC kwa miaka 199.
Kwa kuwa CPO pia ndio wamiliki wa jina la Chelsea FC, wakairuhusu timu itumie jina hilo kwa masharti kwamba, itacheza mechi zake zote za nyumbani kwenye uwanja wao (yaani Stamford Bridge).
*Iwapo timu itamua kuhama na kucheza mechi zake nje ya Stamford Bridge, itapoteza haki za kutumia jina la Chelsea FC*
Na iwapo watataka kuendelea kutumia jina hilo itawalazimu kupeleka maombi yao kwenye CPO ambayo itapiga kura na kupitishwa kwa zaidi ya 75% ya wamiliki wa CPO
CPO ikafanikiwa kuzalisha £1.5m kupitia mauzo ya hisa hadi kufikia 2011. Wakati fulani, John Terry ndiye alikua Rais wa CPO (sina hakika kama alimaliza muda wake au lah).
CPO ndiyo sehemu pekee rahisi ya washabiki kumiliki sehemu ya Chelsea na wanahimizwa kununua hisa kupitia CPO.
*Kama tunataka kum control mrusi na timu yetu, hapa ndio pa kuwekeza kwa nguvu*
Ndipo klabu ikatangaza nia ya kutanua Stamford Bridge ili ikaliwe na mashabiki 55,000.
Kutokana na miundo mbinu inayozunguka uwanja (njia za reli na barabara zinazozunguka uwanja), uwezekano wa kutanua uwanja pembani ukaonekana ni ndoto isiyowezekana.
Mwaka 2011, klabu ikatangaza nia ya kununua eneo la uwanja na uwanja (kutoka kwa CPO). Kikao cha CPO kilipokaa, kilikataa ombi la klabu la kuwauzia mali yake.
Hivyo klabu ilianza kutazama uwezekano mbadala wa kuhama darajani. Tukumbuke kama wangehama darajani bila ridhaa ya CPO, wangepoteza haki za kuitwa Chelea FC. Yaelekea Roman Abramovich alikuwa tayari kwa hilo mwaka 2012.
Kwa bahati nzuri, kituo cha kuzalisha umeme cha Battersea ambacho walipanga kukinunua na kukigeuza uwanja, hawakufanikiwa kukipata, kwani kilinunuliwa na wawekezaji wa Malasyia.
Kati ya mwaka 2012-14, klabu iifanya majaribio mengi sana ya kuhama kutoka darajani, kwa bahati nzuri yote yaligonga mwamba.
Ndipo wakaweka mkandarasi mwelekezi ambaye akagundua kwamba, upanuzi wa Stamford Bridge kufikia watu 60,000 ungewezekana.
Badala ya kutanua pembeni, mshauri mwelekezi huyo alishauri uwanja uchimbwe zaidi kwenda chini, ili majukwaa yaanzie chini zaidi na zile hoteli za bwana Bates zivunjwe ili kupata eneo zaidi.

Mchoro huo ukapitishwa na Mayor wa mji na juzi kizingiti cha mwisho (yule jirani aliyekuwa akidai atazibwa mwanga wa jua), alipoamuliwa kwamba atalipwa fidia na Fulham Council. Bado ana uwezo wa kukata rufaa, lakini hadi hapo, ndoto ya kupata uwanja mkubwa zaidi kwenye eneo lile lile, inaonekana kupata matumaini makubwa


No comments:

Post a Comment