MUALIKO KWAKO SHABIKI WA CHELSEA - Darajani 1905

MUALIKO KWAKO SHABIKI WA CHELSEA

Share This
Mara baada ya kukuletea ufafanuzi juu ya klabu ya Chelsea na umiliki wake juu ya uwanja wa Stamford Bridge ambalo hilo limekuwa likiwashinda mashabiki wengi wa Chelsea kutokuelewa juu ya umilikishwaji wa uwanja huo kwa klabu na timu ya Chelsea ambapo ufafanuzi wake kama unahitaji kuupata, bonyeza hapa

Sasa hapa nakuletea mualiko wa sherehe ya kutimiza miaka 25 ya chombo kisicho cha faida ambacho kiliundwa ili kuumiliki uwanja wa Stamford Bridge pamoja na jina la Chelsea ambao wanajiita Chelsea Pitch Owners (CPO). Huku mgeni rasmi akitajwa kuwa ni mmiliki wa Chelsea wa zamani, Ken Bates ambaye yeye ndiye alihusika kwa kiasi kikubwa kundwa kwa CPO lakini pia ndiye aliyemuuzia Roman Abramovich klabu hiyo.

Sherehe hizo za kufurahia kutimiza miaka 25 zitafanyika mwezi Machi-2018  katika uwanja wa Stamford Bridge katika ukumbi wa Harris Suite huku kiingilio kikiwa paundi 185, paundi 165 na paundi 150 huku wale wanachama wa CPO watapatiwa punguzo.

Ili kujiunga na kupata kitambulisho katika kushiriki katika sherehe hizo, nimekuwekea fomu hapa ili uweze kujiandikisha, bonyeza hapa kuipata fomu hiyo

No comments:

Post a Comment