Unaikumbuka ile mechi ya Chelsea ilipopoteza dhidi ya Man city? unakumbuka jukwaani walionekana mchezaji wa zamani, Michael Ballack na kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani, Hansi Flick?
Sasa unaambiwa moja kati ya mambo ambayo yalimfanya Hansi Flick kusafiri mpaka jijini London ilikuwa ni kukaa chini ana kwa ana na kocha Thomas Tuchel ili kujadili jinsi ya kurudisha makali ya Timo Werner.
Na hivyo makocha hao waliweka mikakati vizuri jinsi ya kurudisha ubora wa nyota huyo haswa kwenye kufumania nyavu, kuanzia kwenye taifa lake mpaka klabuni.
Timo Werner anaweza kushuka uwanjani kwenye mchezo wa kesho pindi taifa lake litakaposhuka uwanjani kucheza dhidi ya Romania kwenye mchezo wa kuwania kufuzu kucheza Kombe la Dunia.
No comments:
Post a Comment