Mzaliwa wa Brazil mwenye uraia wa Italia, Jorginho Frello amekamilisha usajili wake wa kujiunga na Chelsea mchana wa leo akiwa ni mchezaji wa kwanza kusajiliwa na kocha mpya wa klabu hiyo, Maurizzio Sarri.
Jorginho anatajwa kusaini mkataba wa miaka mitano utakaomfanya kulipwa mshahara wa paundi 102,000 kwa wiki.
Chelsea inatajwa kulipa paundi milioni 57 ili kuwapata Jorginho na Maurizio Sarri ambao wote wamesajiliwa kutokea klabu ya Napoli ya nchini Italia ambapo huko waliiongoza klabu ya Napoli kumaliza nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu Italia maarufu kama Serie A.
Kusoma zaidi kuhusu Jorginho, wapi ametokea, asili yake na takwimu zake, bonyeza hapa
Karibu Darajani..
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
No comments:
Post a Comment