Tarehe 17-Juni ndiyo siku maalumu michuano ya kombe la dunia itaanza huko nchini Urusi inamaana zimesalia siku kadhaa kabla ya michuano hiyo kuanza.
Kuelekea kwenye michuano hiyo kumekuwa na mfululizo wa uteuzi qa wachezaji kwa kila timu itakayoshiriki michuano hiyo ambapo kila timu shiriki hutaja nyota 23 ambao wanawachagua ili kuwakilisha mataifa yao kwenye michezo hiyo.
Hii leo kocha wa kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani, Joachim Low amewachagua wachezaji 23 watakaounda timu ya taifa ya Ujerumani huku nyota wa Chelsea, Antonio Rudiger akipata fursa ya kuchaguliwa kwa mara ya kwanza ili kushiriki michuano hiyo.
Rudiger ambaye amecheza michezo kadhaa ya kirafiki kwa ajili ya kujiandaa na michuano hiyo amechaguliwa kama mmoja wa walinzi katika safu ya ulinzi ya timu hiyo ambayo ni mabingwa watetezi.
Kikosi kamili;
Walinda mlango: Manuel Neuer (Bayern Munich), Marc-Andre ter Stegen (Barcelona), Kevin Trapp (Paris St-Germain)
Walinzi: Jerome Boateng (Bayern Munich), Matthias Ginter (Borussia Monchengladbach), Jonas Hector (Cologne), Mats Hummels (Bayern Munich), Joshua Kimmich (Bayern Munich), Marvin Plattenhardt (Hertha Berlin), Antonio Rudiger (Chelsea), Niklas Sule (Bayern Munich)
Viungo: Julian Brandt (Bayer Leverkusen), Julian Draxler (Paris St-Germain), Leon Goretska (Schalke), Ilkay Gundogan (Manchester City), Sami Khedira (Juventus), Toni Kroos (Real Madrid), Mesut Ozil (Arsenal), Sebastian Rudy (Bayern Munich)
Washambuliaji: Mario Gomez (Stuttgart), Thomas Muller (Bayern Munich), Marco Reus (Borussia Dortmund), Timo Werner (RB Leipzig)
Hongera kwake...
No comments:
Post a Comment