Nyota wa zamani wa Chelsea na timu ya taifa ya Uingereza, John Terry anatajwa kutaka kustaafu kucheza soka huku akitoka kumaliza mkataba wake wa mwaka mmoja aliosaini nao na klabu ya Aston Villa ulioisha mwezi Juni mwaka huu.
Nyota huyo anatajwa kujiandaa kustaafu soka ambalo amelitumikia muda mwingi akiichezea klabu ya Chelsea ambayo aliichezea kwa miaka 22 huku akiwa nahodha kwa miaka 13 huku akiweka rekodi na kushinda mataji kibao kabla ya kuachana na klabu hiyo mwaka 2017 na kujiunga na klabu ya Aston Villa.
Kuna vyanzo viwili vimeripoti taarifa mbili tofauti kuhusu taarifa yake ya kustaafu ambapo chanzo chake kimesema mara baada ya kustaafu kwake ataajiriwa na kampuni moja ya kuripotiwa michezo na kufanya kazi kama mchambuzi wakati chanzo kingine kikidai nyota huyo anajiandaa kujiunga katika benchi la ufundi la Chelsea akifanya kazi ya ukocha kwa upande wa mabeki wa klabu hiyo.
Je unadhani huu ni muda sahihi kurejea Chelsea?
No comments:
Post a Comment