Dortmund wazidi kumbania Pulisic - Darajani 1905

Dortmund wazidi kumbania Pulisic

Share This

Klabu ya Chelsea imekatishwa tamaa kwa mara nyengine juu ya kumsajili nyota wa klabu ya Borrusia Dortmund, Christian Pulisic mara baada ya klabu yake kukataa ofa yoyote juu ya kusajiliwa nyota huyo.raia wa Marekani.

Mara ya kwanza ilidaiwa nyota huyo mwenye miaka 19 alisema anatazamia kuondoka klabuni hapo ifikapo mwishoni mwa msimu na sasa klabu yake imekataa ofa yoyote kutoka kwa Chelsea na Bayern Munich ambao nao wanamtaka.

Pulisic hajasaini mkataba mpya klabuni hapo huku mkataba wake wa sasa ukiwa unamalizika mwaka 2020.

No comments:

Post a Comment