Hazard afanya mazungumzo na kocha Sarri - Darajani 1905

Hazard afanya mazungumzo na kocha Sarri

Share This

Kocha Maurizio Sarri ataiongoza Chelsea jioni ya leo katika mchezo wa kwanza wa kimashindano wakati Chelsea itakapopambana dhidi ya klabu ya Manchester city kwenye mchezo wa Ngao ya Hisani ambapo Chelsea anacheza mchezo huu akiwa kama bingwa wa michuano ya Kombe la FA huku Manchester cjty ikiingia kama bingwa wa ligi kuu Uingereza.

Lakini wakati kila mtu akiusubiri mchezo huo, bado kikosi cha wachezaji wa Chelsea hakijakamilika kutokana na tarehe za kurejea klabuni kutokana na mapumziko waliyopewa na klabu kutokana na kushiriki michuano ya Kombe la Dunia kuwa bado kwa wengine lakini kwa wengine ikiwa ni siku ya leo ya tarehe 5-Agosti ndio wanatakiwa warejee klabuni, moja kati ya nyota hao ni Eden Hazard. Lakini kuna taarifa imetolewa na kocha Sarri alipohojiwa kuhusu nyota huyu raia wa Ubelgiji.

"Niliongea na Hazard kupitia simu, hatukuongelea kuhusu mustakabali wake ila aliniomba arejee klabuni siku ya jumatatu badala ya jumapili kama ilivyotakiwa" alisema kocha Sarri kuhusu maongezi aliyoyafanya na winga wa klabu hiyo, Eden Hazard

Hazard na nyota wenzake ambao ni Thibaut Courtois, Michy Batshuayi na Gary Cahill ambao walihusika kwenye mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu wa Kombe la Dunia walipangiwa kurejea klabuni siku ya tarehe 5-Agosti ambayo ndiyo leo jumapili huku nyota mwenzao Ruben Loftus-Cheek alipangiwa pia tarehe hiyo lakini aliamua kurudi kabla ili ajiweke sawa

Bado haijajulikana kama kapewa ruhusa ya kurejea klabuni siku ya jumatatu ambayo pia ni siku ya kurejea kwa nyota waliocheza fainali ya Kombe la Dunia ambao ni N'Golo Kante na Olivier Giroud.

No comments:

Post a Comment