Ni usiku mwengine mzuri, na ni usiku mwengine tunaoenda kuwashuhudia nyota wa kikosi cha Chelsea wakishuka uwanjani kucheza mchezo wa Kombe la Dunia huko nchini Urusi.
Gary Cahill ambaye ni nahodha wa klabu ya Chelsea ataongozana na nyota Ruben Loftus-Cheek wakiiwakilisha timu ya taifa ya Uingereza kucheza mchezo wa mwisho wa hatua ya 16 bora kwa Kombe la Dunia mwaka huu.
Nyota hao ambao walikuwepo kwenye mchezo uliopita wa hatua ya makundi wakati Uingereza ilipomenyana dhidi ya Ubelgiji na kupoteza mchezo huo kwa bao 1-0 wataiongoza timu yao usiku wa leo kucheza dhidi ya Colombia huku ikihitaji ushindi ili ifanikiwe kufudhu hatua ya robo fainali.
Kama nyota hao wakishuhudia timu yao ikishinda mchezo wa leo basi itakamilisha idadi ya nyota watano wa Chelsea kucheza robo fainali mwaka huu.
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
No comments:
Post a Comment