HERI YA KUZALIWA DAMIEN DUFF - Darajani 1905

HERI YA KUZALIWA DAMIEN DUFF

Share This
Wakati Chelsea ikijiandaa kucheza mchezo wake waligi kuu siku ya jumapili dhidi ya Mama site (Man city) kwenye uwanja wa Etihad Stadium unaopatikana kwenye jiji la Manchester, leo tunajikumbusha moja ya mashujaa waliowai kuichezea klabu yetu pendwa ya Chelsea ambapo alitua hapo mwaka 2003 akifanikiwa kucheza misimu yake mitatu ya mafanikio klabuni hapo akishinda mataji mawili ya ligi kuu na taji moja la kombe la ligi ambapo alisajiliwa akitokea klabu ya Blackburn Rovers akisajiliwa kwa dau la paundi milioni 17.

Damien Duff leo anatimiza miaka 39 toka kuzaliwa kwake mwaka 1979 siku kama ya leo huko kwenye jiji la Dublin nchini Ireland na kufanikiwa kushinda mataji kadhaa kama mwanasoka.

Nyota huyo kwa sasa ni kocha wa klabu ya Shamrock Rovers huku akiwa na historia kubwa aliyoijenga klabuni Chelsea na hata kwenye taifa lake la Ireland akiichezea michezo 100 na kuifungia magoli nane. Toka alipotua klabuni Chelsea mwaka 2003 aliichezea Chelsea michezo 81 na kuifungia magoli 19 na kuondoka klabuni hapo mwaka 2006.

No comments:

Post a Comment