ALICHOKISEMA ANTONIO CONTE KUELEKEA Man city vs CHELSEA - Darajani 1905

ALICHOKISEMA ANTONIO CONTE KUELEKEA Man city vs CHELSEA

Share This
Chelsea itakuwa na mchezo wake wa ligi kuu Uingereza mwishoni mwa wiki hii, ambapo watasafiri tena mpaka kwenye jiji la Manchester ambapo huko walicheza mchezo wao uliopita dhidi ya Manyumbu (Man utd) ambapo Chelsea ilipoteza kwa magoli 2-1. Na wiki hii watakuwa tena kwenye jiji hilo lakini safari hii watamenyana na majirani wa klabu hiyo, Mama site (Man city).

Kuelekea kwenye mchezo huo wa jumapili, kocha Antonio Conte amefanya mkutano na waandishi wa habari akitoa taarifa kuelekea kwenye mchezo huo, na hapa nakuletea baadhi ya aliyoyaongea kocha huyo.

Alipoulizwa juu ya jinsi gani anaufikiria mchezo huo dhidi ya klabu hiyo alisema, "Wanacheza soka safi, soka ambalo linawafanya kuwa bora mpaka kuwa ngumu kutambua udhaifu wao upo wapi. Na hiyo ndio faida ya kuwa na kocha bora na ukampatia fungu la kutosha la kufanyia usajili, matokeo yake ndio yanakuwa haya"

Alipoulizwa juu ya majeruhi watakaoukosa mchezo huo, kocha Antonio Conte alijibu "David Luiz, Ethan Ampadu pamoja na Tiemoue Bakayoko ndio watakaukosa mchezo huo wa jumapili kwa Barkley ameanza mazoezi na timu na amekuwa sawa na anaweza akaungana nasi katika mchezo huo wa jumapili"

Hayo ni baadhi tu ya aliyoyaongea wakati ikiwa inajiandaa kupambana na klabu hiyo iliyo kileleni mwa msimamo wa ligi kuu Uingereza huku ikiiacha Chelsea kwa alama 22.

No comments:

Post a Comment