LEWANDOWSKI AGOMBANA MAZOEZINI, AWAITA CHELSEA - Darajani 1905

LEWANDOWSKI AGOMBANA MAZOEZINI, AWAITA CHELSEA

Share This
Chelsea inatajwa kumfukuzia nyota raia wa Poland ambaye ni mshambuliaji wa klabu ya Bayern Munich, Robert Lewandowski ambaye kwa sasa ana miaka 29. Ambapo pia inatajwa kuna upinzani kutoka kwa klabu inayofundishwa na kocha wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho ambaye kwa sasa ni kocha wa Manyumbu (Man utd) ambao na wao wanatajwa kumfukuzia nyota huyo.

Lakini kuna habari njema kwa Chelsea katika kumuwania nyota huyo ambapo inaelezwa nyota huyo aligombana akiwa mazoezini na mchezaji mwenzake ambaye walishawai kuichezea Borrusia Dortmund kwa pamoja, Matt Hummels ambapo huenda hiyo ikamhamasisha nyota huyo afikirie kuondoka klabuni hapo.

Inaelezwa wakati nyota hao walipokuwa mazoezini, Lewandowski alikuwa akicheza timu moja na mlinzi huyo raia wa Ujerumani, wakati mpira alipoupata Lewandowski akaukokota kisha kusimama na kuanza kufunga kamba za viatu huku akiwa na mpira, ndipo nyota mwenzake klabuni hapo, Tolliso ambaye kwa muda walijigawanya kama wachezaji wa timu tofauti akamfata na kuuchukua mpira kisha kufunga kiurahisi, ambapo kwa tukio hilo lilimkasirisha Hummels na kuanza kumfokea Lewandowski kwa kuleta mzaha wakiwa mazoezini na mshambuliaji huyo akamjibu. Taarifa zinadai mpaka nyota hao wanatoka mazoezini, hakuna aliyemuongelesha mwenzake.

Kwa sababu hiyo, huenda ikamfanya nyota huyo kufikiria kuondoka klabuni hapo haswa ukizingatia amecheza kwa muda mrefu na kuna uwezekano akataka kuondoka ili kutafuta changamoto mpya.

No comments:

Post a Comment