EDEN HAZARD AINGIA KWENYE UCHEZAJI BORA FEBRUARI - Darajani 1905

EDEN HAZARD AINGIA KWENYE UCHEZAJI BORA FEBRUARI

Share This
Kama ilivyoada kila tunapojaaliwa na mwenyezi Mungu muumba mbingu na nchi kuingia mwezi mwengine, huwa kunatolewa tunzo kwa wale waliofanya vizuri katika mwezi uliopita. Na tumetoka mwezi Februari na kuingia mwezi Marchi kwa hiyo ligi kuu Uingereza imeandaa tunzo za mwezi wote wa Februari na kuchagua wachezaji waliofanya vizuri katika mwezi huo.

Eden Hazard, nyota wa Chelsea mwenye miaka 27 ambaye ni raia wa Ubelgiji naye amefanikiwa kuingia kwenye kinyang'anyiro cha kuwania tunzo ya mchezaji bora kwa mwezi Februari akiiongoza vyema klabu yake katika michezo ya ligi kuu kwa mwezi huo.

Katika mwezi huo, aeiongoza Chelsea katika michezo mitatu ya ligi kuu huku akifanikiwa kuiongoza kushinda mchezo mmoja dhidi ya West Bromwich ambapo mwenyewe alifunga magoli mawili na kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo. Lakini pia katika mwezi huo akifunga magoli matatu na kuteneza nafasi 11.

Wengine anaoshindana nao katika kipengele hicho;

  • Sergio Aguero-Man city
  • Moussa Dembele-Tottenham
  • Pascal gross-Brighton
  • Glenn Murray-Brighton
  • Mohammed Salah-Liverpool
  • Xherdan Shaqiri-Stoke city


No comments:

Post a Comment