FRANK LAMPARD KUPEWA UKOCHA CHELSEA - Darajani 1905

FRANK LAMPARD KUPEWA UKOCHA CHELSEA

Share This
Kuna taarifa zimetolewa na chombo kimoja cha habari nchini Uingereza zikidai kuwa mmiliki wa Chelsea anajiandaa kumpa nafasi mchezaji wa zamani wa klabu hiyo, Frank Lampard kuwa kocha wa kikosi cha timu ya Chelsea Fc ambayo ndio klabu inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza na ligi nyengine.

gwiji huyo wa soka aliyecheza kwa mafanikio makubwa klabuni Chelsea na kufanikiwa kutwaa mataji kadhaa yakiwemo ya ligi kuu ambayo alitwaa mataji matatu matatu lakini pia akicheza klabuni hapo kwa miaka 13 na kufanikiwa kuwa mfungaji bora wa muda wote klabuni hapo amekuwa akisaidiana na makocha wa timu za vijana ya klabuni Chelsea akiwafundisha vijana wa klabu hiyo kwenye uwanja wa mazoezi wa Cobham kwa muda sasa, lakini pia amekuwa kwenye mafunzo ya kusomea ukocha akitauta leseni la kiwango cha A anatajwa kuungana na benchi la ufudni la Chelsea ambapo atakuwa vhini ya kocha Antonio Conte kama kocha msaidizi wa kikosi cha timu ya wakubwa.

Taarifa zinadai kuwa mmiliki, Abramovich anakaribia kumpa kibarua hicho gwiji huyo akitazamia kumuandaa kuwa kocha wa Chelsea kwa miaka ya baadae ambapo kwa sasa leseni yake ya ukocha haimruhusu kufundisha timu kama kocha mkuu kwenye michuano ya Ulaya ikiwemo na michuano ya klabu bingwa barani humo ama ligi ya Europa.

No comments:

Post a Comment