NYOTA WA ARSENAL KUTUA CHELSEA KISA UBAHILI WA WENGER - Darajani 1905

NYOTA WA ARSENAL KUTUA CHELSEA KISA UBAHILI WA WENGER

Share This
Toka kutoka kwake kwenye klabu ya Afc Bournemouth, amekuwa na msimu mzuri klabuni Arsenyani (Arsenal) akionekana kuwa na mhimili mzuri katika nafasi ya kiungo, lakini toka klabu hiyo impate Henrikh Mkhitaryan, nyota huyo anaonekana kupoteza nafasi yake katika kikosi cha kwanza cha klabu hiyo, ni kiungo raia wa Uingerza, Jack Wilshere. Na sasa anatajwa kushindwana na masharti na klabu yake na kuna uwezekano klabu ya Chelsea ikatumia nafasi hiyo kumvuta nyota huyo.

Taarifa zinadai kuwa klabu ya Arsenyani imemwambia nyota huyo kuwa akubali kupunguziwa mshahara wake kwa asilimia 25 ya mshahara anaopokea kwa sasa ambapo anavuta paundi 120,000 kwa kila wiki kama anataka kuendelea kubaki klabuni hapo. Lakini masharti hayo yanaonekana kuwa magumu kwa Wilshere ambaye kiasili ni mzaliwa kabisa wa jiji la London ambapo klabu hiyo inatokea, na ukizingatia wanaotoka mbali na hapo kama Pierre Aubameyang, Mesut Ozil pamoja na Mkhitaryan wanapokea mshahara mkubwa kuliko yeye na hawajapewa sharti hilo.

Sasa Chelsea inatajwa kuingia kwenye nia ya kumsajili kiungo huyo na kuna uwezekano mkubwa wa kukubali kutua klabuni hapo kutokana na mapenzi yake ya kutaka kubaki kwenye jiji la London, ambalo ndilo jiji mwenyeji kwake. Klabu ya West Ham nayo inatajwa kumuwania.

No comments:

Post a Comment