FAQ - Darajani 1905

FAQ

FAQ ni kifupi cha maneno ya kiingereza yaani Frequentry Asked Questions ikimaanisha maswali ya mara kwa mara, na hapa nimekuwekea kipengele hiki kutokana na watu wengi kuuliza maswali mengi yaihusuyo klabu ya Chelsea ambapo maswali mengi yamekuwa yakijirudiarudia, na hapa nakuletea mfululizo wa maswali hayo na majibu yake kiufasaha.

Swali; Chelsea ilianzishwa lini?
Jibu; Klabu ya Chelsea ilianzishwa rasmi tarehe 10-Marchi-1905 huko nchini Uingereza kwenye jiji la London na mwanzilishi wa klabu hiyo alikuwa Gus Mears, mfanyabiashara ambaye aliianzisha klabu hiyo kutokana na kuumiliki kwake uwanja wa Stamford Bridge huku akijikuta hana timu anayoimiliki. Kwa maana hiyo akaamua kuianzisha klabu hiyo ili iitumie uwanja huo wa Stamford Bridge.


Swali; Je uwanja wa Stamford Bridge unamilikiwa na klabu au ni uwanja wa serikali?
Jibu; Uwanja wa Stamford Bridge ulioanzishwa au kufunguliwa mwaka 1877 unamilikiwa na mashabiki wa Chelsea waliounda taasisi yao huru ya Chelsea Pitch Owners (CPO) ambapo wanalimiliki jina la Chelsea FC pamoja na uwanja wa Stamford Bridge. Kusoma zaidi, bonyeza hapa

Swali; Taji la kwanza la Chelsea lilikuwa ni lipi?
Jibu; Napozungumzia mataji kwa hapa nazungumzia yale mataji yanayofamika kimataifa ambapo kwa Chelsea taji lake la kwanza lilitwaliwa mwaka 1955 ambapo lilikuwa taji la ligi daraja la kwanza (ligi kuu Uingereza) ambapo ilikuwa chini ya kocha Ted Drake.
Kama kuna maswali yatakayoonekana kuleta utata au kama kuna maswali utahitaji yapatiwe ufumbuzi kutoka Darajani 1905, basi usisite kututumia ujumbe kupitia mawasiliano yetu.

Kuwasiliana nasi, bonyeza maneno yenye rangi ya bluu kupata mawasiliano yetu. Darajani 1905

No comments:

Post a Comment