Jana tulianza uchambuzi kuhusu michezo ya Chelsea katika michuano ya ligi kuu Uingereza kwa msimu wa 2018-2019 ambapo tuliutazama mchezo wa kwanza wa Chelsea ambapo itakuwa ugenini kumenyana dhidi ya Huddersfield.
Leo tunaendelea na uchambuzi ambapo tutaugusia mchezo wa pili ambapo Chelsea itakuwa nyumbani kumenyana dhidi ya Arsenal.
Mchezo huu utakuwa mchezo wa kusisimua ambapo kocha mpya wa Arsenal atakumbana na klabu kigogo mfululizo huku akianza mchezo wa kwanza kwa kumenyana dhidi ya Manchester city.
Mchezo huu utachezwa siku 18 mara baada ya klabu hizo kukutana katika mchezo wa kirafiki wa kujiandaa na msimu mpya ambapo watamenyana kwanza kama mchezo wa kirafiki, kisha Chelsea itacheza mchezo wa ngao ya hisani kisha baadae kucheza dhidi ya Huddersfield kisha baadae Chelsea kumenyana na washika bunduki.
Kihistoria klabu hizo zilikutana kwa mara ya kwanza mwaka 1907, miaka miwili toka Gus Mears kuianzisha Chelsea na Chelsea ikaitandika Arsenal magoli 2-0 katika mchezo wa Ligi Daraja la kwanza ambao kwa sasa ndo unaitwa Ligi kuu Uingereza na ukizungumzia michezo ya ligi kuu, katika michezo 10 ya ligi kuu ya mwisho ambayo klabu hizo zilimenyana, Chelsea imepoteza mchezo mmoja tu, lakini ikiondoka na ushindi katika michezo 5 na kutoa suluhu michezo minne.
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
No comments:
Post a Comment