MASHABIKI WA CHELSEA WAFURAHI KUUMIA KWA BAKAYOKO - Darajani 1905

MASHABIKI WA CHELSEA WAFURAHI KUUMIA KWA BAKAYOKO

Share This
Mara baada ya kocha wa Chelsea, Antonio Conte kutoa taarifa juu ya kukosekana kwa mchezaji, Tiemoue Bakayoko na Marcos Alonso kuwepo kwenye mchezo wa Chelsea dhidi ya Barcelona utakaochezwa siku ya jumanne tarehe 20-Februari ambapo Chelsea itakuwa nyumbani Stamford Bridge katika mchezo wa klabu bingwa Ulaya kwa hatua ya 16 bora, kumekuwa na maoni mengi yakitolewa juu ya kukosekana kwa Bakayoko katika mchezo huo, ambapo wengi wa mashabiki hao wakieleza kufurahishwa na taarifa hizo.

Kusoma taarifa hizo, bonyeza hapa

Nyota huyo raia wa Ufaransa anaonekana kushindwa kuonyesha ubora aliokuwa nao pindi alipoisaidia klabu ya As Monaco kutwaa taji la ligi kuu Ufaransa msimu uliopita na huku akitajwa kama mmoja wa viungo wakabaji bora kwa mwaka 2017, alisajiliwa Chelsea kwa dau la paundi milioni 34 na mpaka sasa anatajwa na mashabiki wengi wa Chelsea kuwa mmoja ya wachezaji wanaocheza soka bovu huku akicheza mchezo wake wa mwisho dhidi ya Watford ambapo mchezo huo alipata kadi nyekundu kwa dakika za mwanzoni kabisa.
Kupitia mtandao wa Twitter mashabiki hao wametoa hisia zako juu ya taarifa hizo huku wengi wakisema kukosekana kwake haitoidhuru Chelsea na badala yake Chelsea itazidi kuwa imara.

Je kwa maoni yako ni yapi juu ya kiungo huyu?

No comments:

Post a Comment