Bila shaka mchezo wa kesho wa nusu fainali ya Kombe la Dunia kati ya Ufaransa dhidi ya Ubelgiji utakuwa mchezo utakaotazwa na mashabiki wengi haswa wa Chelsea kutokana na nyota wake watano kuhusika kwenye mchezo huo.
N'Golo Kante na Olivier Giroud kwa upande wa Ufaransa wakati kwa upande wa Ubelgiji kutakuwa na Eden Hazard,Michy Batshuayi na Thibaut Courtois.
Kuna kauli nyingi zimetolewa na nyota hao wakiwazungumzia nyota wenzao. Kusoma kuhusu Olivier Giroud alichokiongea kuhusu Thibaut Courtois, bonyeza hapa. Kusoma alichokiongea Eden Hazard kuhusu N'Golo Kante, bonyeza hapa.
Hatimaye tena Olivier Giroud ametoa kauli nyengine kuhusu nahodha wa Ubelgiji, Eden Hazard akisema "Hazard ni mtu mzuri sana, na ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa. Tukiwa uwanjani (klabuni Chelsea) mimi nahitaji msaada wake naye anahitaji msaada wangu"
Hazard na Giroud wamekuwa wakitumika kwa pamoja katika michezo mingi toka Giroud asajiliwe na Chelsea akitokea Arsenal kwenye dirisha dogo la usajili la mwezi Januari.
Je nani ataibuka kuwa bingwa? usisahau kuandika maoni (comment) yako na kusambazia (share) kwa wengine.
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
No comments:
Post a Comment