Kocha Antonio Conte kufika klabuni Chelsea kusimamia mazoezi ya nyota wa klabu hiyo hii leo licha ya kuhusishwa kuondoka kunaweza kufungua milango ya mambo mengine kuendelea.
Hiyo ni kutokana na kuripotiwa mara kadhaa kwamba nyota wanaotakiwa na klabu hiyo wanashindwa kukamilisha sajili zao kutokana na kutoelewa nani atakuwa kocha kwa msimu ujao.
Hakuna uthibitisho kamili kwamba kocha huyo ataendelea kuwa na Chelsea kwa msimu mwengine lakini hilo halikumfanya nyota kiungo raia wa Ivory Coast, Jean Michael Seri kufikia makubaliano binafsi na klabu ya Chelsea.
Mwandishi wa habari wa tovuti ya Yahoo ameripoti kwamba nyota huyo mwenye miaka 26 anayeichezea klabu ya OGC Nice ya nchini Ufaransa anataka kutimikia Uingereza kucheza soka lake lakini amefikia makubaliano binafsi na klabu ya Chelsea licha ya Arsenal kuonyesha nia ya kumtaka na kubwa analolisubiri kwasasa ni kukamilika mazungumzo kati ya klabu yake na klabu ya Chelsea. Thamani ya nyota huyo inatajwa kufikia paundi milioni 35.
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
No comments:
Post a Comment