Mara baada ya Chelsea kumalizana dhidi ya Liverpool pale Darajani siku ya tarehe 29-Septemba, sasa klabu hiyo itasafiri mpaka St. Mary's stadium ambapo huko itamenyana dhidi ya Southampton.
Tarehe 6-Oktoba, Chelsea itamenyana dhidi ya Southampton katika mchezo utakaokuwa wa kulipiza kisasi kwa klabu hiyo ambayo msimu uliomalizika walipoteza michezo miwili mfululizo dhidi ya Chelsea, wakipoteza kwenye ligi kuu kisha kwenye nusu fainali ya Kombe la FA shukrani kwa goli bora la nyota kibabu wa Chelsea, Olivier Giroud akitumia pasi njema kutoka kwa Eden Hazard na kuwapiga chenga kipa na walinzi wake na kufunga goli safi lililosaidia Chelsea kucheza fainali ya michuano hiyo.
Lakini pia shukrani kwake tena katika ule mchezo wa ligi kuu ambapo aliingia kama mchezaji wa akiba wakati Chelsea ikiwa nyuma kwa magoli 2-0 na baadae kufunga magoli mawili akishirikiana na Eden Hazard kuipa ushindi Chelsea wa magoli 2-3.
Turudi kwenye uchambuzi, Chelsea itaendelea kuhitaji ushindi kwenye mchezo huu na huenda ikaendelea kumtumia Giroud ambaye anaonekana kuiweza sana klabu hiyo ya Southampton au wanajiita The Saints. Kwenye mchezo huo, Chelsea itaingia kwa kujiamini haswa kutokana na kushinda michezo yote mitatu kwa msimu uliopita dhidi ya klabu hiyo.
Tukirudi kwenye historia, michezo 44 Chelsea imefanikiwa kupata ushindi dhidi ya Southampton wakati ikipoteza kwenye michezo 30 huku michezo 28 ikimalizika kwa sare. Mchezo wa kwanza kwa klabu hizo kukutana uliisha kwa sare kwenye michuano ya Kombe la FA. Lakini Chelsea inapata nguvu kutokana na kutopoteza mchezo wowote wala kutoa suluhu dhidi ya klabu hiyo toka mwaka 2015. Toka mwaka huo, klabu hizo zimekutana mara sita, na mara zote Chelsea imeondoka na ushindi.
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
No comments:
Post a Comment