Mohammed Salah anavyoungana na Darajani 1905 - Darajani 1905

Mohammed Salah anavyoungana na Darajani 1905

Share This

Siku kadhaa zilizopita nilizindua kampeni maalumu niliyoipatia jina la Charity For The Blues iliyochini ya blog hii ya Darajani 1905 ambayo ni maalumu kwa mashabiki wa Chelsea lakini pia kwa wapenzi wa soka ili kuifanya jamii yetu ifaidike kwa ushabiki wetu wa soka uwe na faida kwa jamii tunazotokea ambapo tulipanga kuanza kwa kuchangia damu kwa hiyari ambapo uchangiaji huo tulipanga tuanze nao kwenye hospitali ya wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam siku ya tarehe 19-May ambayo itakuwa ni siku ya mwisho kwa klabu yetu pendwa ya Chelsea kushuka uwanjani ili kukamilsha msimu wa 2017-2018 ambapo itacheza mchezo wa kombe la FA dhidi ya Manchester united. Lakini pia blog hii itakuwa inatimiza miezi 6 toka kuzaliwa kwake ambapo ilizaliwa tarehe 19-Desemba-2017.

Kwa kuwa uchangiaji huu wa damu hautokua kwa ajili ya mashabiki wa Chelsea tu bali pia na mashabiki wengine ambao ni watani zetu na hata hii blog imekuwa ikitembelewa na hata wasiokua mashabiki wa Chelsea basi hapa nakuletea simulizi fupi ya nyota wa klabu ya Liverpool, Mohammed Salah ambaye alishawai kupita Chelsea nia ni kukuonyesha kwa kiasi gani soka linavyoweza kuleta amani na furaha mahali panapoonekana hapafai kama alivyofanya Didier Drogba ambaye ukamilisho wa sehemu ya pili nitakuletea kesho jumanne kwenye blog hiihii. (kusoma sehemu ya kwanza, bonyeza hapa)

Mo Salah amekuwa aking'aa kwa Liverpool pengine kuisaidia jamii ya alipotokea kumemfanya azidi kufanya vizuri.

Salah amezaliwa katika familia ya watoto wanne akiwa mtoto mkubwa akitokea kijiji cha Nagrig jimbo la Gharbia maili 80 kaskazini mwa mji mkuu wa Misri, Cairo.

Katika kijiji hicho cha Nagrig Mo amenunua gari ya wagonjwa ya kwanza kijijini kwake pamoja na vifaa vya gharama kwa ajili ya hospitali, mashine moja aliyonunua inahudumia zaidi ya watu 50 kwa siku.

Mo Salah anapokea mshahara wa pauni 90,000 kwa wiki katika klabu ya Liverpool.

Mbali na hospitali anatumia takribani pauni 3500 kila mwezi kuzisaidia familia ambazo haziwezi kujiendesha kwa kuwanunulia vyakula na mahitaji mengine.

Pia Salah anajenga kituo cha vijana, shule ya wasichana ambayo itafanya watoto wa kike wa Nagrig kutolazimika kwenda kusoma mbali , pamoja na kituo cha afya.

Na kila mtu anayeoa kwenye kijiji chake humnunulia vitu vya ndani kuwasaidia kuanza maisha ya ndoa.

Mke wa Salah pia ametoka katika kijiji hicho, wameoana mwaka 2013, wana mtoto mmoja wa kike anayeitwa Makka.

Na kitendo cha kushangaza zaidi ni pale mwizi alipovamia nyumbani kwa kina Salah na kukamatwa, baba yake akataka ampeleke mahakamani lakini Salah akasema asamehewe, akampa mwizi huyo fedha na kisha akamsaidia kupata kazi.

Katika kijiji hicho Salah amepachikiwa jina la "Mtengeneza furaha".

Tajiri mmoja ambaye alikuwa rais wa klabu ya Zamalek, alimpa kiasi fulani Salah baada ya kuiwezesha Misri kufuzu kombe la Dunia 2018, lakini hakuzichukua hela hizo na kuagiza zitumike katika matumizi ya Hospitali katika kijiji chake cha Nagrig.

Ama kweli ni Mfalme wa Egypt na ule msemo wa utakavyotoa ndivyo utakavyopata unaonekana dhahiri kwa Sheikh Salah.

Lakini nikujuze kitu ambacho labda haujawai kukijua? N'Golo Kante analipwa mshahara mkubwa kwa wiki kuliko Salah, Kante analipwa paundi 110,000 wakati Salah analipwa 90,000

Shukrani; Worldsports kutoka Instagram

No comments:

Post a Comment