Chelsea yaingia sokoni kusaka mshambuliaji, yatua kwa nyota wa Lyon - Darajani 1905

Chelsea yaingia sokoni kusaka mshambuliaji, yatua kwa nyota wa Lyon

Share This

Chelsea inatajwa na gazeti la nchini Ufaransa kuwa ni klabu ya mwisho kumfukuzia nyota na mshambuliaji wa klabu ya Olympique Lyon ya nchini Ufaransa, Nabil Fekir ambaye pia anatajwa kufukuziwa na baadhi ya klabu vigogo barani Ulaya.

Gazeti la L'Equippe linaitaja klabu ya Chelsea kumfukuzia mshambuliaji huyo ambaye amekuwa na msimu mzuri na kuonyesha uwezo mkubwa akiwa kwenye klabu hiyo ambayo mpaka sasa ameshaichezea michezo 33 na kuifungia magoli 22.

Chelsea inatajwa kukaribia kumpoteza mshambuliaji wake, Alvaro Morata ambapo taarifa zinazagaa kuwa nyota huyo anakaribia kutimkia Juventus ambapo tayari ashamalizana nayo kwa mahitaji binafsi.

No comments:

Post a Comment