Chelsea ilipata ushindi katika mchezo wake wa raundi ya 36 ya msimu wa 2017-2018 ya ligi kuu nchini Uingereza hapo jana ambapo ilicheza dhidi ya Liverpool na kufanikiwa kuondoka na ushindi wa bao 1-0 na kuondoka na alama zote tatu na kuifanya Chelsea ifikishe alama 69 na kufufua matumaini yake ya kucheza michuano ya klabu bingwa barani Ulaya kwa msimu ujao.
Mara baada ya matokeo hayo, nyota wa Chelsea ametoa muonekano wake na nini anakitazama kwa sasa kutokana na nafasi iliyokua nayo Chelsea katika kupambania kufudhu kucheza michuano ya klabu bingwa barani Ulaya maarufu kama UEFA Champions League.
"Kwa sasa lengo letu ni kushinda michezo iliyobaki na kufanikiwa kufudhu kuingia kwenye klabu nne za juu kwenye msimamo, na kama tukicheza kama tulivyocheza kwenye michezo mitatu iliyopita basi tunaweza kufaidika kwa kupata jambo zuri mwishoni mwa msimu"
"Acha tuendelee kuwa na matumaini ya kupata kitu kikubwa. Sote tunacheza kwa kushirikiana na tunafanikiwa kucheza kama tunavyocheza, mwisho wa mchezo unajisikia vyema na unajiona mwenye furaha" alisema nyota huyo raia wa Ubelgiji.
Lakini pia katika tukio jengine ambalo hili limeshuhudiwa kutokana na ujumbe wa video alioutuma nyota huyo kupitia mtandao wa Instagram, nyota huyo alionekana kwenye video huyo akicheka na kusema hakuna nafasi hiyo pale alipoulizwa kama kuna nafasi kwake kuungana na klabu ya Manchester united inayonolewa na kocha wa Chelsea wa zamani, Jose Mourinho.
No comments:
Post a Comment