Katika sehemu iliyopita, tuliona sehemu ya mahojiano aliyofanyiwa mchezaji wa zamani wa Chelsea na timu ya taifa ya Ivory Coast, Didier Drogba akifanyiwa mahojiano na mwandishi wa gazeti la The Telegraph ambaye alisafiri umbali mrefu ili kukutana na gwiji huyo ambaye kwa sasa ni mmiliki na mchezaji wa klabu ya Phoenix ya nchini Marekani. Kusoma sehemu ya 1, bonyeza hapa
Na sasa tunaingia sehemu ya pili ambapo mwandishi huyo alifunga safari kutoka kwenye mji mkuu wa Ivory Coast, Abidjan na kwenda mahali alipozaliwa na kukuria nyota huyo.
Sasa tuendelee..
Wachezaji wengi haswa maarufu wamekuwa wakiutumia umaarufu wao kwa kufanya mambo makubwa ikiwamo kufungua miradi mbalimbali ndani ya miji mikubwa au kufadhili sehemu fulani lakini hakuna aliyeweza kuisimamisha nchi yake kutoka kwenye dimbwi la machoz. Drogba ni mtu muhimu sana kwa watu wa Ivory Coast sio kutokana na umaarufu wake lakini sababu kubwa ni kutokana na kutumika kama kipaza sauti akiitetea jamii yake.
Tukiwa njiani kuelekea nyumbani ambapo nyota huyo alizaliwa na kulelewa nje kidogo ya mji mkuu wa Abidjan, nyota huyo anasema yeye ni kama raia wa kawaida tu na anaweza kuishi hata kama akiwa hana pesa kutokana na kulelewa kwenye maisha ya kawaida kabisa na ndio maana anazitumia mali zake ili kuirejesha kwenye jamii iliyomlea na kumfanya afikie hapo alipo.
Lakini kwa kufupisha nyota huyo alikamilisha mahojiano na mwandishi huyo kwa kuongea maneno yanayoonyesha kwa kiasi gani ana uzalendo na jamii iliyomlea na kwa nchi yake ambapo alimaliza akisema "Nimeshinda mataji mengi kwenye maisha yangu yote ya soka, lakini hakuna jambo kubwa na kuu kwangu kama kuisaidia jamii yangu kupata amani tena. Najivunia sana katika hilo maana hii leo hatuhitaji tunzo au medali yoyote kufurahia ndani ya nchi yetu ya Ivory Coast"
Didier Drogba kwa sasa pia ana taasisi binafsi anayoiongoza ambapo anatoa misaada haswa nchini Ivory Coast ambapo mpaka sasa ameshafanikiwa kusaidia ujenzi wa miradi nbalimbali ikiwemo shule aliyoijenga kupitia taasisi hiyo ya Didier Drogba Foundation.
*********
Bila kusahau zimesalia siku 11 kabla ya mashabiki wa Chelsea na wapenzi wote wa soka kukutana pale Hospitali ya serikali ya Temeke jijini Dar es Salaam ili kuifanya jamii yetu ifaidike kwa kupenda kwetu soka ambapo tutachangia damu kwa hiyari
#CharityForTheBlues
No comments:
Post a Comment