Chelsea kumrudisha Musonda Jr mwishoni mwa msimu? - Darajani 1905

Chelsea kumrudisha Musonda Jr mwishoni mwa msimu?

Share This

Raia wa Ubelgiji ambaye ni mchezaji halali wa Chelsea, Charly Musonda Jr anafikiriwa kupunguziwa muda wake wa mkopo ambao anautumikia akiwa na klabu ya Celtic ya nchini Scotland.

Chelsea inatajwa kutaka kumpunguzia mchezaji huyo ambae alijiunga kwa mkopo wa miezi 18 ambayo ni sawa na mwaka 1 na nusu ili kuichezea kwa mkopo klabu hiyo ingawa mpaka sasa ameshindwa kuitumikia vyema klabu hiyo iliyochini ya kocha Brendan Rodgers ambaye aliwai kuwa kocha wa vijana klabuni Chelsea.

Chelsea inatajwa kutokuwa na furaha kwa jinsi nyota huyo anavyokosa nafasi kwenye kikosi cha Celtic ambapo inamtuhumu kocha huyo kuwa na ubaguzi kwa wachezaji wa Chelsea ambapo kama utakuwa na kumbukumbu zilizoshiba aliwai pia kumkosesha nafasi Victor Moses pindi nyota huyo alipojiunga kwa mkopo klabuni Liverpool ambapo kocha huyo alikuwa akiifundisha klabu hiyo.

Chelsea inataka kumrejesha Musonda Jr mwishoni mwa msimu huu ambapo nyota huyo atakuwa amekamilisha miezi 6 (kati ya miezi 18 aliyotakiwa atumike kwa mkopo) akiwa kwa mkopo klabuni Celtic ambapo tangu ajiunge nayo ameichezea michezo sita tu tangu ajiunge nayo katika dirisha dogo la usajili la mwezi Januari.

No comments:

Post a Comment