Chelsea yaisubiri FIFA kupata mustakabali wa ubingwa wa dunia - Darajani 1905

Chelsea yaisubiri FIFA kupata mustakabali wa ubingwa wa dunia

Share This

​Chelsea inaendelea kusubiri uamuzi kutoka shirikisho la soka la dunia, FIFA juu ya lini na wapi michuano ya Klabu bingwa ya Dunia itafanyika.


Hatua hiyo inakuja mara baada ya Japan kujiondoa kwenye mpango wa kuandaa michuano hiyo iliyotakiwa kufanyika mwezi Desemba mwaka huu.


Lakini hali ilivyo mpaka sasa, kuna uwepo wa mapendekezo mbalimbali ya lini michuano hiyo itaanza na wapi kutatakiwa kuchukua nafasi ya kuandaa michiano hiyo ambayo Chelsea inashiriki kama bingwa wa bara la Ulaya.


Nchi ya Afrika Kusini, Qatar na Brazil zimekuwa zikihusishwa kuwania nafasi hiyo.


No comments:

Post a Comment