Kumekuwa na tetesi nyingi zikimhusisha ocha wa Chelsea, Antonio Conte kuondoka klabuni hapo huku makocha kadhaa wakitajwa kumrithi kocha huyo muitaliano klabuni Chelsea. Baadhi ya makocha waliowai kuhusishwa na mpango huo wa kuingia klabuni Chelsea ni pamoja na kocha wa sasa wa klabu ya Juventus, Massimiliano Allegri ambaye pia aliingia klabuni Juventus akichukua nafasi ya Antonio Conte ambaye alijiunga na timu ya taifa ya Italia ili kuinoa timu hiyo.
Mara baada ya tetesi nyingi na taarifa kibao kuenea juu ya kocha huyo kurithi mikoba kwa mara nyengine tena ya kocha Antonio Conte, kocha huyo amefunguka rasimi juu ya tetesi hizo.
"Ninaifundisha klabu kubwa na nina mkataba wa kuwa hapa mpaka mwaka 2020. Nina furaha ya kuwa hapa" alisema kocha huyo ambaye naye ni raia wa Italia huku akiwa anaifundisha klabu ya Italia.
Makocha wengine wanaohusishwa kuchukua nafasi ya Conte kikosini Chelsea ni pamoja na Diego Simeone aliyeipatia mafanikio makubwa klabu ya nchini Hispania, Atletico Madrid na kocha Maurizio Sarri ambaye kwa sasa anaifundisha klabu ya Napoli.
MRITHI WA CONTE ATOA MAJIBU YA KUTUA KWAKE CHELSEA
Share This
Tags
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment