HERI YA KUZALIWA ANTONIO RUDIGER - Darajani 1905

HERI YA KUZALIWA ANTONIO RUDIGER

Share This
Nyota wa Chelsea, Antonio Rudiger leo ni kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa ambapo alizaliwa tarehe kama ya leo mwaka 1993 huko jijini Berlin nchini Ujerumani na hii leo anatimiza miaka 25.

Katika kusheherekea kumbukumbu yake ya kuzaliwa, hapa nakuletea historia fupi inayomhusu nyota huyu ambaye mpaka sasa ameshaichezea Chelsea michezo 35 na kuifungia magoli 3 akisajiliwa hapo katika dirisha kubwa la usajili lililopita kwa dau la paundi milioni 27.

Nyota huyo kama nilivyokueleza hapo juu kwamba alizaliwa kwenye jiji la Berlin nchini Ujerumani na klabu yake ya kwanza kuichezea ikiwa ni klabu yaVfB Sperber Neukolln ambaye alianza kuichezea akiwa na miaka 7 lakini maisha yake ya soka kama mchezaji kamili aliyaanza akiwa kwenye klabu ya VfB Stuttgart II ambapo alicheza huko kwenye timu ya pili kabla ya baadae kupandishwa mpaka timu ya wakubwa hiyo ikiwa mwaka 2012 na kufanikiwa kutolewa kwa mkopo na kujiunga na klabu ya As Roma ambayo baadae ilimsajili kabisa na kuwa mchezaji wa klabu hiyo.

Alicheza hapo As Roma kwa mafanikio makubwa na kufanikiwa kuwa moja ya wachezaji mahiri klabuni hapo akicheza kama mlinzi wa kati akiwa na ufundi mkubwa wa kutoa pasi za mwisho ambapo mpaka anaondoka klabuni hapo alifanikiwa kuichezea michezo 35 huku akitengeneza mabao manne katika msimu wake wa mwisho klabuni hapo.

Chelsea ndipo ikavutiwa na nyota huyo na hatimaye mwezi Julai mwaka jana, Chelsea ikatangaza kumsajili nyota huyo huku akipewa mkataba wa miaka mitano.

Hivi ulishawai kujiuliza kwanini nyota huyu ni raia wa Ujerumani ila ana ngozi nyeusi ambayo inaaminika ni ngozi yenye asili ya Afrika? Ipo hivi, nyota huyo ana asili ya barani Afrika ambapo mama yake ni raia wa Sierra Leone huku baba yake akiwa ni mjerumani kabisa.

Hongera Antonio Rudiger.




No comments:

Post a Comment