KITAMBO; PESA ILIIPA USHINDI CHELSEA KUIFUNGA AC MILAN - Darajani 1905

KITAMBO; PESA ILIIPA USHINDI CHELSEA KUIFUNGA AC MILAN

Share This
Ukifuatilia kumbukumbu zina utamu wake na muda mwengine zinaweza kukuacha ukiwa unacheka tu. Hivi unajua kama Chelsea ilishawai kushinda kutokana na sarafu? Ndiyo sarafu ya pesa iliwafanya watoke kimasomaso. Naamini kabisa historia nyingi uliwai kuzisikia lakini hii itakuwa ni mpya na ngeni kwako.

Ilikuwa msimu wa 1965-1966 ambapo Chelsea ilikuwa inashiriki kombe la Inter-Cities Fair ambapo ilitakiwa kumenyana dhidi ya Ac Milan, Chelsea ya miaka hiyo ndio ilikuwa na magwiji kama Peter Osgood ambaye tunamuita Mfalme wa Stamford Bridge, ilikuwa na Bobby Tambling na nahodha wa miaka hiyo alikuwa Ron Harris.

Mchezo wa kwanza ulichezwa katika uwanja wa Ac Milan ambapo Chelsea ilisafiri mpaka nchini Italia ili kumenyana na klabu hiyo na ikapoteza kwa magoli 2-1 ambapo mchezo wa marudiano ulikuwa unamaanisha Chelsea inarudi Stamford Bridge na kuikaribisha Ac Milan ambapo mchezo huo, Chelsea haikutaka kuwaangusha mashabiki wake na ikafanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-1.

Kwa matokeo hayo yalimaanisha matukio ya jumla ni 3-3, kwa maana hiyo hakuna aliyefanikiwa kufudhu kucheza hatua nyengine kutokana na matokeo kufungana. Ndipo ikaamuliwa sarafu itumike, wakaitwa manahodha wa timu mbili, sarafu ikarushwa ili kuchagua mchezo wa tatu uchezwe wapi kama ni nchini Italia au uchezeke tena Stamford Bridge. Sarafu ikarushwa na nahodha wa Ac Milan akafanikiwa kuchagua upande sahihi, na mchezo wa tatu ambao ndio ungeamua nani wa kufudhu kucheza hatua inayofata.

Sasa Chelsea ikabidi isafiri mpaka nchini Italia ambapo huko sasa ndipo kulitokea sababu inayonifanya leo nikuletee historia hii.

Mara baada ya kufika huko, mchezo ukachezwa na ukaisha kwa suluhu ya 1-1, ambapo kwa matokeo hayo hayakumaanisha timu yoyote kufanikiwa kufudhu kucheza hatua inayofata.

Sasa nini kifanyike, anaeleza Tambling, "ilitakiwa turudi vyumbani, kwenye vyumba vya kubadilishia nguo, na kumuacha Ron Harris (aliyekuwa nahodha wa Chelsea) akiwa bado uwanjani. Kiukweli tulichoka, na ingekuwa ngumu kuendelea kucheza dakika za nyongeza. Basi ikaamuriwa manahodha wafike katikati ya uwanja na sarafu kuamuliwa kurushwa ambapo wakati natoka kwenye chumba cha kubadilishia nguo nilimuona Ron Harris akiruka kuonyesha kushangilia"

Kushangilia kwa nahodha huyo kulimaanisha Chelsea ilifanikiwa kufudhu kucheza hatua ifuatayo kwa ushindi wa sarafu.

 Sasa kwanini nimekuletea historia hii, siku kama ya leo mwaka 1966 ndio ulichezeka mchezo huo na mpaka leo imeshapita miaka 52.

No comments:

Post a Comment