Historia ya maisha ya Hakim Ziyech - Darajani 1905

Historia ya maisha ya Hakim Ziyech

Share This


Alizaliwa tarehe 19-Machi mwaka 1993 huko kitongoji cha Dronten nchini Uholanzi, kitongoji ambacho mpaka sasa kinakadiliwa kuwa na watu 50,000.

Hakim Ziyech akiwa na mama yake

Ziyech alikuwa ni mtoto wa nane kati ya familia ya mzee mwenye uraia wa Uholanzi na mama mwenye asili ya nchini Morocco, alikuwa mtoto wa mwisho wa familia na kutimiza idadi ya watoto wa kiume watano na wakike watatu.

Hakim Ziyech akiwa na dada yake

Akiwa ana  miaka 8 alijiunga kwa mara ya kwanza  na timu ya soka iliyopo kwenye kitongoji chao cha Dronten na hapo alizichezea klabu mbili tofauti kabla  ya baadae kujiunga na klabu yenye hadhi ya juu, klabu ya SC Heerenvee.

Hakim Ziyech alipokuwa mchezaji wa SC Heerenvee

Lakini kabla ya kujiunga na klabu hiyo alipokuwa ana miaka 10 akawa shuhuda wa kifo cha baba yake ambacho kilisababisha mama kuwa tegemeo kubwa la familia na ikasababisha kwa  kiasi kikubwa familia kuyumba kiuchumi.


Alipojiunga na klabu hiyo ya Heerenvee mwanzoni hakuwa na mwenendo mzuri ingawa alionekana mwenye kipaji kikubwa, alijiunga na makundi ya vijana wabaya mpaka pale nyota wa zamani wa soka ambaye pia ana asili ya Morocco ingawa alikuwa anaishi Uholanzi alipoanza kumsimamia akigundua kipaji chake na kumtazama kama mchezaji mwenye kipaji bora sana.

Aziz Doufikar (waliosimama ni mtu wa pili kutoka kushoto) akiwa na timu ya vijana sambamba na Hakim Ziyech (waliosimama ni mtu wa pili kutoka kulia)

Jitihada za nyota huyo aliyeitwa Aziz Doufikar zikazaa matunda na hatimaye Ziyech akaanza kurudi kwenye mstari.

Kiwango kikaongezeka na akazidi kujitambulisha kwenye soka la Uholanzi.

Mwaka 2014, alikamilisha uhamisho wake wa kujiunga na FC Twente ya hukohuko Uholanzi ambako huko alijiunga akiwa ana miaka 21.

Hakim Ziyech akiwa na timu ya taifa ya Morocco kwenye Kombe la Dunia mwaka 2018.

Mwaka 2015, akachagua kuitumikia timu ya taifa ya Morocco kutokana na asili ya mama yake ingawa soka lake lote la ujanani kwenye timu za taifa aliitumikia timu ya taifa ya Uholanzi.

Mwaka 2016, alikamilisha uhamisho wake wa kujiunga na Ajax Amsterdam ambapo hapo ndipo palipomtambulisha zaidi mpaka pale Chelsea ilipokamilisha uhamisho wake unaotajwa  kuwa na thamani ya paundi milioni 35.


Takwimu zinamtaja nyota huyo kuwa na uwezo mkubwa wa kutengeneza nafasi na akiwa hatari zaidi katika boksi la timu pinzani.

No comments:

Post a Comment