Mkutano wa kocha Frank Lampard kuelekea Chelsea dhidi ya Man utd - Darajani 1905

Mkutano wa kocha Frank Lampard kuelekea Chelsea dhidi ya Man utd

Share This
Mkutano wa kocha Frank Lampard kuelekea mchezo wa Chelsea dhidi ya Man utd:


Alipoulizwa kuhusu wachezaji walio na majeraha, amesema "Christian Pulisic bado hajawa sawa, ni leo tu amefanya mazoezi na kikosi cha vijana. Ruben (Loftus-Cheek) pia hatokuwa sawa kwa ajili ya huu mchezo. Tammy pia ataangaliwa kama atakuwa sawa."

Alipoulizwa kuhusu usajili wa Hakim Ziyech, amesema "Ni mchezaji mzuri na naamini ataleta ubunifu mpya. Ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa na nafikiri alikuwa sehemu kubwa ya kuifanya Ajax ifanye vizuri kwenye klabu bingwa Ulaya mwaka jana."

Alipoulizwa kuhusu Kepa Arrizabalaga amesema "Mwitikio umekuwa mzuri kwake kama nilivyotegemea. Sikuwai kukaa nae chini kuzungumza nae sana lakini nafikiri kuanzia sasa natakiwa kulitimiza."


"Kumweka benchi yalikuwa maamuzi ya kutaka kila mchezaji awe na tahadhari. Ata nami nilipokuwa mchezaji niliwai kukutana na hali aliyokutana nayo. Nataka kila mchezaji apambane akicheza kwa tahadhari."

Hayo ni machache kati ya mengi yaliyozungumzwa kwenye mkutano wa leo kati ya kocha na waandishi wa habari.

1 comment:

  1. How to make money from sports betting and casino games
    A casino table gives you more than just a chance to win, and febcasino it's free. How to make kadangpintar money from online gambling. งานออนไลน์ The casino is also known as a

    ReplyDelete