Didier Drogba alivyookoa maisha ya wengi {Sehemu 1} - Darajani 1905

Didier Drogba alivyookoa maisha ya wengi {Sehemu 1}

Share This
Leo nakuletea moja ya makala aliyowai kufanyiwa moja ya magwiji klabuni Chelsea, Didier Drogba ambaye ni raia wa Ivory Coast ambapo alifanyiwa na mwandishi kutoka gazeti la The Guardian la nchini Uingereza.
Kubwa alilolisema "Alex, njoo Abidjan. Hautojutia" kiukweli mcheza soka anapokwambia usafiri kwa ndege tena usafiri kwa umbali mrefu mpaka ukatue Afrika Magharibi ili mfanye mahojiano, inakuwa ni kama jambo lisiloingia akilini. Lakini Didier Drogba hakuwa mchezaji anayejiona na niliamini nitamfanyia mahojiano mtu mkarimu na mahojiano yetu yatakua yakikarimu.
Muda mfupi nilipofanikiwa kutua kwenye mji mkuu wa nchi aliyozaliwa Didier Drogba, nchi ya Ivory Coast. Na ndipo hapo nilipopata wasaa wa kufahamu kwa kiasi gani Drogba alikuwa nyota. Karibu kila mitaa na kona za nyumba zilikuwa zimejaa matangazo ya simu na bidhaa nyengine zikiwa na utambulisho wake.
Ilikuwa haina ubishi kuwa Drogba ndiye alikuwa ni sura ya nchi, alama ya nchi, shujaa wa vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini Ivory Coast. Je ilikuwaje na aliwezaje kuleta amani nchini kwao?
Vita ya wenyewe kwa wenyewe ilikuwa ikiendelea nchini Ivory Coast kwa miaka mitano na ndipo alipoisaidia timu yake ya taifa kufudhu kucheza kombe la dunia kwa mwaka 2006 zilizotakiwa kuchezwa nchini Ujerumani ukirudi nyuma kidogo mpaka mwezi Oktoba mwaka 2005, Drogba alichukua kipaza sauti huku akiwa kwenye chumba cha kubadili nguo huku akiwa amezungukwa na wachezaji wenzake, alipiga magoti mbele ya televisheni ya taifa. Aliziomba pande mbili zilizoanzisha mapigano hayo kuachana na vita hiyo na ndani ya wiki moja maombi yake yakakubaliwa. Na vita vikamalizwa.
"Kila mchezaji alikuwa anachukia kilichokua kinaendelea nchini na kufanikiwa kwetu kufudhu kucheza kombe la dunia lilikuwa ni jambo kubwa na muhimu kwetu"
Mpango wa kukamilika kwa maswala ya amani na mapatano kwa pande hizo mbili zilizoanzisha vita hiyo ya Ivory Coast ilianza kuonekana wakati timu ya taifa ya wanawake ya nchini Ivory Coast wanaojiita jina la utani la White Elephants au Tembo Weupe walipocheza mchezo wa kufudhu wa kombe la Afrika maarufu kama African Nations Cup ambapo walicheza dhidi ya Madagascar katika moja ya miji yenye nguvu nchini Ivory Coast, jiji la Bouake ambalo lilikuwa chini ya moja wa kundi la waanzilishi wa vita hiyo ambapo linapatikana km 300 kutoka mji mkuu wa Abidjan.
"Kuwaona viongozi wa waanzilishi wa vita hiyo kwa pande zote wakiwa pamoja na wanaimba nyimbo ya taifa lilikuwa ni jambo kubwa na muhimu. Nilijisikia kama Ivory Coast imezaliwa tena na ina tabasamu jipya" alisema Didier.
Mwandishi wa makala hii anasema ukubwa wa Didier Drogba nchini kwao alitamani audhihirishe kupitia kwa wananchi wa nchini humo, na ikabidi awafate wananchi na kuwauliza juu ya gwiji huyo, mwandishi anasema alipowafanyia mahojiano alishangazwa na raia wengi nchini humo wanavyompenda gwiji huyo jambo lililomfanya mwandishi amgeukie Drogba na kumuuliza tena kwanini hajawai kuelezea juu ya ushawishi mkubwa alionao nchini kwao katika vyombo vya habari vya nchini Uingereza ambapo alikuwa anatimiza majukumu yake nchini humo kama mchezaji wa Chelsea.
"Sikuwa nikifikiri kuwa nilihitajika kufanya hivyo kwamba nieleze kwa kiasi gani naheshimika ndani ya Afrika. Najua ni kipi nimekisimamia na mtazamo wangu ni upi na hilo ndio jambo la muhimu zaidi"
"Kiukweli huwa haliniumizi kichwa na kunisumbua akili pale mtu alipokua akihoji na kunikosoa nikiwa uwanjani. Watu wanaojua mengi kuhusu mimi wanajua kwanini nipo ivi" alisema gwiji huyo alipoulizwa juu ya kwanini hakutaka kuutumia ukubwa wake ili kuwaonyesha watu kuwa ana heshima kubwa.
Haya ni mahojiano mafupi ambapo kama unataka kujua kipi kilijiri pale mwandishi huyo alipofunga safari mpaka mahali alipozaliwa na kukuria nyota huyo. Tukutane jumanne ya tarehe 08-May mwaka huu kwa ajili ya sehemu ya pili
**************
Nia na sababu ya kukuletea makala haya ya gwiji huyu ni kukuonyesha kwa kiasi gani mchezo wa mpira wa miguu au soka unavyoweza kubadilisha maisha kuyatoa kwenye vita mpaka kwenye amani ambapo nami pamoja na mashabiki wa Chelsea tunataka kuyabadilisha maisha ya wazazi wetu, ndugu jamaa na marafiki waliopo mahospitalini kwa hitaji la damu kuwatoa kwenye maisha ya kupambania maisha yao na kuwafanya kuwa na amani kwa kuwachangia kwa hiyari kupitia kampeni ya Charity For The Blues ambapo tutaanza kwa kuchangia damu kwa hiyari siku ya tarehe 19-May pale hospitali ya serikali ya Temeke jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment