Alvaro Morata aeleza maisha yake ya kila siku Chelsea - Darajani 1905

Alvaro Morata aeleza maisha yake ya kila siku Chelsea

Share This
Hapa nakuletea mahojiano aliyoyafanya mshambuliaji wa Chelsea, Alvaro Morata ambaye alifanyiwa mahojiano na televisheni maalumu ya klabu ya Chelsea akiulizwa juu ya ratiba na nini anakifanya kila siku pindi anapofika kwenye uwanja wa mazoezi wa Chelsea maarufu kama Cobham Stadium.
Chelsea TV; Huwa unatumia muda gani kufika Cobham kabla ya mazoezi na mambo gani huwa unayafanya kabla ya kuelekea mazoezini?
Alvaro Morata; Tunatakiwa kufika Cobham saa moja kabla ya mazoezi kuanza nami kwa kawaida huwa nafika saa moja na nusu kabla ya mazoezi kuanza. Jambo la kwanza kulifanya huwa nnapata chakula cha kifungua kinywa ambapo huwa ninakula pamoja na baadhi ya wachezaji wenzangu na baada ya hapo huwa nafanya mazoezi ya viungo kidogo au nnatibiwa kidogo ili kujiweka sawa nikiwa na mtaalamu wa viungo. Kisha ntatoka na kwenda kupiga mswaki, na kuosha uso wangu na kuviandaa viatu vyangu pamoja na vitu vyangu ili kwenda uwanjani. Muda mwengine huwa tunakuwa na mkutano wa timu kabla ya kutoka nje, ambapo hapo huwa tunapata wasaa wa kuangalia video za timu nyengine. Na tukimaliza hapo tukifika uwanjani huwa tunafanya mazoezi kwa juhudi kubwa.

Chelsea TV; Huwa unakula nini katika mlo wako wa kifungua kinywa?
Alvaro Morata; Inategemea. Muda mwengine huwa nnakula maziwa mtindi pamoja na matunda, au parachichi lakini huwa naangalia kwa siku hiyo najisikiaje. Siku nyengine huwa natumia kahawa
Chelsea TV; Huwa unavaa 'jersey' gani wakati wa mazoezi?
Alvaro Morata; Mara zote huwa inategemea na hali ya hewa ipo vipi, kwa mfano, kama kukiwa kuna jua sana huwa navaa 'pensi' fupi pamoja na 't-shirt' lakini kama kukiwa kuna mvua huwa navaa vazi maalumu kunikinga na mvua.
Chelsea TV; Je una aina(jozi) ngapi ya viatu vya michezo (njumu) unazozitumia kwa msimu mzima?
Alvaro Morata; Ni ngumu kulijibu hilo maana sijazihesabu, ila kwa kukadiria ni kama aina 20 za viatu. Mara zote huwa napenda kuvaa aina moja ya viatu nnavyovitumia kwenye mazoezi na uwanjani kwenye mchezo, lakini ukizungumzia aina ya viatu kutokana na utofauti wa rangi kama sikosei nina kama aina nne au tano za viatu vinavyotofautishwa kwa rangi na ukizungumzia juu ya viatu kutokana na makampuni basi nina aina 12 mpaka 15 ya viatu vinavyotengenezwa na makampuni tofauti.
Chelsea TV; Je ni aina gani ya hali ya hewa huwa unaipenda ukiwa kwenye mazoezini?
Alvaro Morata; Napenda kuwe na anga la bluu lakini kusiwe na jua kali sana maana ni ngumu sana kufanya mazoezi kwenye hali ya joto.
Chelsea TV; Huwa unafanya mazoezi yako binafsi mara baada ya mazoezi ya pamoja au kabla?
Alvaro Morata; Ndiyo. Kabla ya mazoezi ya pamoja, kama sijaenda kukutana na mtaalamu wa viungo basi nitatumia muda wa ziada nikiwa kwenye chumba cha mazoezi (gym) nikijiweka sawa.
Chelsea TV; Chakula chako cha mchana huwa unakula nini?
Alvaro Morata; Kiukweli baada ya mazoezi huwa nakula pasta. Pastani chakula muhimu sana kwetu wachezaji haswa kama unataka kuwa sawa. Kisha ili kupata nguvu huwa nakula nyama au samaki. Kama tukifanya mazoezi mengi tukiwa kwenye chumba cha mazoezi (gym) basi nitakula nyama nyingi ambayo inakuweka sawa haswa baada ya kutoka kwenye mazoezi ya chumba cha mazoezi (gym), na kama tukifanya mazoezi ya kukimbia sana basi nitakula sana samaki, lakini yote kwa yote huwa inategemea na aina ya mazoezi tuliyofanya. Tukiwa Cobham huwa tuna aina ya vyakula tofauti.
Chelsea TV; Je aina ya chakula unachokula huwa kinabadilika kutokana na aina ya mchezo utakaofata?
Alvaro Morata; Ndiyo, nina uhakika. Kama siku mbili kabla ya mchezo huwa ninakula kiasi kidogo cha 'chocolate' au kitu kinachofanania na icho lakini huwezi kufanya hivyo muda mfupi kabla ya mchezo kuanza. Kabla ya mchezo inabidi uwe ngangari na imara kwa asilimia zote, hakikisha unakuwa na nguvu na unakula kiafya.
*******MWISHO

No comments:

Post a Comment