Kumbe Mbappe ndiye aliyeichokoza Chelsea - Darajani 1905

Kumbe Mbappe ndiye aliyeichokoza Chelsea

Share This
Wiki iliyopita nilikuletea taarifa inayomhusu mchezaji aliyenunuliwa kwa dau nono zaidi duniani, Neymar akiichokoza klabu ya Chelsea mara baada ya kuripotiwa taarifa kuwa nyota na winga huyo ameiambia klabu ya Real Madrid kuwa kama wanataka ajiunge na klabu hiyo basi ifanye bidii ili kuwasajili nyota kadhaa akiwemo na mchezaji wa Chelsea, Eden Hazard. Ili kuisoma habari hiyo, bonyeza hapa

Lakini sasa nyota mwenzake wa klabu ya PSG, Kylian Mbappe naye amejitokeza na kuichokoza Chelsea kama alivyofanya mchezaji mwenzake.

Mbappe alifanyiwa mahojiano na chombo kimoja cha habari na kusema PSG ili iwe bora basi inahitaji impate N'Golo Kante kutoka Chelsea. Nyota huyo amesema maneno hayo ambayo ni kama yanawachochea viongozi wa klabu hiyo ya PSG ili waweze kumsajili kiungo huyo ambaye amekuwa muhimili mzuri katika safu ya kiungo ya Chelsea.

Mbappe na Kante wamekuwa karibu haswa kutokana na wote wawili kuichezea timu moja ya taifa, timu ya Ufaransa ambapo mahusiano yao mazuri kwenye timu hiyo kumemfanya nyota huyo kutamani mchezaji arejee nchini kwao Ufaransa ambapo aliondoka kwenye ngazi ya klabu mwaka 2015 akitokea klabu ya Caen.

Lakini Kante mwenyewe ametajwa kukataa kuondoka Chelsea na anapenda kusalia kuwa mchezaji wa Chelsea kwa msimu mwengine.

No comments:

Post a Comment