Chelsea yatoa suluhu, yajitilia ugumu kufudhu klabu bingwa Ulaya - Darajani 1905

Chelsea yatoa suluhu, yajitilia ugumu kufudhu klabu bingwa Ulaya

Share This

Chelsea inashindwa kupata ushindi katika mchezo wake wa muhimu dhidi ya Huddersfield mara baada ya kutoka sare ya 1-1 usiku huu katika uwanja wa Stamford Bridge.

Chelsea ilihitaji kupata ushindi katika mchezo huo ili ijiweke kwenye hatua nzuri ya kufudhu kushiriki michuano ya klabu bingwa barani Ulaya kwa msimu ujao ambapo kwa sare hiyo inaifanya kufikisha alama 70 zinazoifanya klabu hiyo kuwa na nafasi finyu ya kufudhu michuano hiyo kwa msimu ujao.

Mchezo kwa ufupi;
Goli la Chelsea lilifungwa dakika ya 62 na mlinzi na winga wake wa kushoto, Marcos Alonso ambapo mpira ulimbabatiza usoni na kuingia golini na kufanya matokeo kuwa 1-1 mara baada ya Chelsea kutanguliwa kwa goli la mapema baada ya kipindi cha pili kuanza.

Kidunchu;
Chelsea iliingia ikiwa na lengo la kushambulia sana na kutafuta goli la mapema lakini ni kama bahati haikuwa upande wa Chelsea lakini pia ugumu ukiongezeka kutokana na mpango waliokuja nao wapinzani ambapo wao walihitaji kuondoka na sare ili iweze kujiepusha kushuka daraja na hata ukiangalia goli walilolipata limefungwa kutokana na maamuzi mabaya ya mwamuzi ambapo winga Willian alikuwa akikokota mpira lakini akachezewa vibaya akizungukwa na wachezaji watatu wa Huddersfield ambapo wakatumia kosa hilo kupiga mpira mrefu na kuwafanya kufunga goli laini huku Caballero akijaribu kuzuia lakini kwa vile alitoka nje ya 18 basi hakutakiwa kuudaka mpira.

Mabadiliko;
Kocha Antonio Conte aliamua kufanya mabadiliko katika kikosi cha leo tofauti na kilichocheza mchezo uliopita dhidi ya Liverpool ambapo ametumia mfumo wa 3-4-3 huku kwa nafasi ya ushambuliaji akiwatumia Pedro, Willian Borges pamoja na Alvaro Morata wakati kwenye kikosi kilichocheza dhidi ya Liverpool aliwatumia Olivier Giroud pamoja na Eden Hazard ambao leo wote wameingia kama wachezaji wa akiba.

Kwa upande wa kiungo kwenye mchezo wa leo amewatumia Davide Zappacosta, Cesc Fabregas, N'Golo Kante pamoja na Marcos Alonso wakati kwenye mchezo uliopita alitumia viungo watano ambapo kwa nafasi ya Zappacosta kuliwa na Victor Moses wakati Tiemoue Bakayoko akikamilisha idadi ya viungo watano.

Wakati kwa nafasi ya ulinzi amefanya mabadiliko kwa kumtumia Andreas Christensen ambae kwenye mchezo uliopita nafasi yake ilichezwa na Gary Cahill wakati kwa nafasi ya mlinda mlango alitumika mlinda mlango nambari mbili, Willy Caballero wakati kwenye mchezo dhidi ya Liverpool alitumika Thibaut Courtois.

Hitimisho;
Mpaka sasa mbaya wa Chelsea anabaki kuwa Liverpool ambapo atakayefanikiwa kufudhu kucheza michuano ya klabu bingwa kwa msimu ujao atajulikana siku ya michezo ya kufunga msimu wa 2017-2018 siku ya jumapili ya tarehe 13-May ambapo Chelsea inatakiwa ihakikishe inaondoka na ushindi kwenye mchezo wa ugenini dhidi ya Newcastle wakati huku Liverpool inatakiwa apoteze dhidi ya Brighton & Hove kwenye mchezo ambao Liverpool watakua nyumbani. Hali inayofanya iwe ngumu kwa Chelsea kufanikiwa kuipata nafasi hiyo haswa kutokana na ugumu wa Liverpool kupoteza tena akiwa nyumbani. Ingawa kwenye soka kila kitu kinawezekana.

No comments:

Post a Comment