NI FAINALI YA CHELSEA vs Man City LEO MCHANA - Darajani 1905

NI FAINALI YA CHELSEA vs Man City LEO MCHANA

Share This
Wakati leo Chelsea ikiwa inatimiza miaka 113 toka kuanzishwa kwake, lakini pia kupitia timu ya vijana ya akademi ya klabu hiyo Chelsea U16, leo itakuwa uwanjani kupambana katika mchezo wa fainali ya ligi kuu Uingereza kwa umri huo wa vijana chini ya miaka 16 ambapo klabu hiyo itakuwa nyumbani kumenyana dhidi ya Manchester city U16.

Mchezo huo wa fainali ambao utaamua ni nani atakuwa bingwa wa michuano hiyo utapigwa katika uwanja wa mazoezi wa Chelsea maarufu kama Cobham Stadium na utachezwa saa 14:00 kwa saa za Afrika mashariki.

No comments:

Post a Comment