Nyota wa Chelsea, Trevoh Chalobah amefanikiwa kusaini mkataba mpya klabuni Chelsea ambapo hapo jana alikamilisha kusaini mkataba wa miaka mitatu na nusu wa kuendelea kusalia klabuni Chelsea na kuwa nyota wa hapo.
Trevoh Chalobah ambaye ni mdogo wa nyota wa zamani wa Chelsea, Nathaniel Chalobah ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Watford amefanikiwa kusaini mkataba huo mara baada ya kuwa na msimu mzuri klabuni Chelsea akiwa ni mmoja wa mazao ya akademi ya klabu hiyo huku akifanikiwa kuteuliwa kwa ara ya kwanza kuingia kwenye kikosi cha kwanza cha Chelsea huku akifanikiwa kuwa mchezaji wa akiba kwa mara ya kwanza tangu kufika klabuni hapo.
Amekuwa akiiongoza vyema klabu ya vijana ya Chelsea mpaka kufanikiwa kufudhu kucheza hatua ya robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya kwa vijana ambapo juma lijalo watasafiri mpaka bchini Hispania kumenyana dhidi ya Real Madrid katika mchezo huo wa robo fainali.
CHELSEA YAMPA KINDA WAKE MKATABA MPYA
Share This
Tags
# Chelsea Usajili
# Chelsea Youth
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Youth
Labels:
Chelsea Usajili,
Chelsea Youth
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment