"....ANAFAA KUWA KOCHA WA CHELSEA" - Darajani 1905

"....ANAFAA KUWA KOCHA WA CHELSEA"

Share This
Mpaka sasa hakuna kinachoeleweka juu ya kocha wa Chelsea, Antonio Conte kama ataendelea kuwa kocha wa Chelsea au ataachana na klabu hiyo ambapo hali inatajwa kwamba kocha huyo haonekani kuendelea kuifundisha klabu hiyo licha ya kupata mafanikio katika msimu wake wa kwanza klabuni Chelsea.

Mengi yanatajwa na mengi yanaelezwa lakini kocha huyo mara zote alipokuwa anaulizwa juu ya kuendelea kubaki kwenye klabu hiyo amekuwa akikiri kwamba ana furaha na bado anataka kubaki klabuni hapo.

Kocha wa zamani wa Barcelona, Luis Enrique ni moja ya makocha wanaotajwa kwa karibu kutakiwa na klabu ya Chelsea ili kuwa mrithi wa kocha Antonio Conte katika klabu hiyo.

Mchambuzi wa soka raia wa Hispania, Guillem Balague nae alieleza juu ya uwezekano wa kocha huyo kutua klabuni Chelsea mwishoni mwa msimu "Naamini Luis Enrique anachokiwaza kwa sasa ni kutua ligi kuu Uingereza, lakini kiukweli jambo hilo halipo katika aamuzi yake. Nimesikia Arsenal wanatajwa kumtaka pia, lakini naamini hakuna ofa yoyote iliyotumwa kwa kocha huyo kutoka Arsenal"

"Chelsea na PSG wote wamekuwa wakitajwa kumtaka, lakini naamini katika kuendana kwa mifumo kati ya kocha huyo basi nadhani Chelsea ataendana nayo sana. Sio klabu inayotazamia sana kujijenga, ni klabu inayotaka ushindi na kushinda mataji kama alivyofanya hivyo akiwa na Barcelona." alisema mchambuzi huyo raia wa Hispania.

Je undahani hili ni chaguo sahihi kwa Chelsea?

No comments:

Post a Comment