ANTONIO CONTE ATOA NENO KUHUSU UBORA WA BAKAYOKO - Darajani 1905

ANTONIO CONTE ATOA NENO KUHUSU UBORA WA BAKAYOKO

Share This
Mashabiki wengi wa Chelsea wamekuwa wakimlalamikia nyota wa klabu hiyo ambaye ni raia wa Ufaransa, Tiemoue Bakayoko huku wakiamini kwamba hakustahili kucheza Chelsea, huku wengine wakinukuliwa wakisema maneno ya kuonyesha kwamba walifurahi nyota huyo kuwa nje katika michezo baadhi mara baada ya nyota huyo kupata majeraha.

Lakini sasa nyota huyo anakaribia kurudi uwanjani mara baada ya kuuguza majeraha yake kwa muda kidogo ambapo hajacheza toka mchezo ambao Chelsea ilipoteza mbele ya Watford katika mchezo ambao Bakayoko alitolewa kwa kadi nyekundu mara baada ya kuonyeshwa kadi za njano mara mbili.

Kocha Antonio Conte ameulizwa juu ya nyota huyo na nini anakiwaza kuhusu nyota huyo ambaye anapata shutuma nyingi kutoka kwa mashabiki.

"Kama kufurahi kupata kwake majeruhi, sio kwamba nitafurahi kwa majeruhi yake, ila kupata muda wa kujifunza mengi juu ya makosa alioyafanya kwenye mchezo dhidi ya Watford. Na sasa amerudi mazoezini na tayari amehaanza mazoezi na timu kwa wiki nzima. Lakini msisahau, Baka ni kijana mdogo sana, ana miaka 22 tu. Bado ana muda wa kupambana zaidi na kurudi kwenye ubora wake na kuwa msaada kwa Chelsea"

Na alipoulizwa kama bado ana imani na nyota huyo ambaye amekuwa akicheza nafasi ya kiungo sambamba na N'golo Kante, kocha huyo alisema "Ndiyo, nina imani nae. Yote kwa sababu, usisahau kama tuna viungo wanne tuu. Ni lazima niwaamini viungo wangu, ni lazima niwaamini wahezaji wangu na kuwaonyesha nini timu inataka kutoka kwao" alisema kocha huyo raia wa Italia.

Je wewe nawe una imani na Bakayoko?


No comments:

Post a Comment