Kuelekea kwenye mchezo huo, kama ilivyoada hapa nakuletea habari muhimu unazopaswa kuzijua kuelekea kwenye mchezo huo ambao unazikutanisha klabu za watani wa jadi kutokana na wote kuishi kwenye jiji hilo la London.
Habari muhimu;
Chelsea: Mara baada ya kuukosa mchezo uliopita kutokana na dharura aliyokuatana nayo akiwa mazoezini, nyota wa Chelsea, N'golo Kante leo atakuwepo uwanjani kupambana na kuisaidia klabu yake kupata alama tatu muhimu ambazo kama wakifanikiwa kuzipata basi itafanikiwa kupunguza pengo la alama ili kuingia kwenye klabu nne za juu katika msimamo wa ligi kuu.
Lakini David Luiz, Ethan Ampadu na Tiemoue Bakayoko watakuwa nje ambapo kwa upande wa Bakayoko ameshaanza mazoezi lakini hakuna uhakika kwamba kocha anaweza kumpa nafasi katika mchezo wa leo haswa kutokana na kutoka majeruhi.
Crystal palace; Nyota wake Wilfred Zaha pamoja na Mamadou Sakho wanaweza kuwa uwanjani kuisaidia klabu yao katika mchezo huu ara baada ya kuwa nje kutokana na majeraha lakini pia fosu-Mensah naye atarudi uwanjani mara baada ya kuukosa mchezo uliopita ambapo klabu hiyo ilimenyana dhidi ya Manchester united, klabu ambayo ilimpeleka kwa mkopo klabuni hapo. Ila nyota kama Joel Ward, Scott Dann, Yohan Cabaye, Ruben Loftus-Cheek, Jason Puncheon, Bakary Sako, Connor Wickham na Julian Speroni wote wataukosa mchezo huu.
Mwamuzi; Anthony Taylor ndiye atakuwa mwamuzi wa leo, ambaye mpaka sasa ameshakuwa mwamuzi katika michezo 29 huku akitoa kadi za njano 110 na kadi nyekundu 3. Toka mwaka 2012 mpaka kufikia leo mwamuzi huyo amehusika kwenye michezo 19 akiwa kama mwamuzi wakati Chelsea ikiwa uwanjani huku katika michezo hiyo Chelsea imeshinda michezo 10 na ikipoteza michezo 2.
Mechi zilizopita;
Chelsea; WWDLL
Crystal Palace; DDLLL
Rekodi; Katika michezo 51 ambayo klabu hizo zilishuka uwanjani kumenyana, Chelsea imeshinda michezo 24 huku ikipoteza michezo 12 na kutoka suluhu michezo 15.
Muda; Mchezo huo utachezwa saa 08:30 usiku (saa 20:30) kwa saa za Afrika Mashariki
No comments:
Post a Comment