HII NDIO SABABU ILIYOMFANYA SALAH AONDOKE CHELSEA - Darajani 1905

HII NDIO SABABU ILIYOMFANYA SALAH AONDOKE CHELSEA

Share This
Nyota wa klabu ya Liverpool, Mohammed Salah aliwai kupita klabuni Chelsea akitokea klabu ya FC Basel ambapo alicheza Chelsea kipindi iko ikiwa chini ya kocha Jose Mourinho ingawa alionekana ni ngumu kwake kutoboa katika kipindi iko na hivyo kuuzwa kwenda kwenye klabu ya As Roma ambayo alipata nayo mafanikio na sasa amesajiliwa na kuwa na msimu mzuri klabuni Liverpool.

Mara baada ya mafanikio yake kumekuwa na mfululizo mkubwa wa maswali watu wakijiuliza kwanini Jose Mourinho alimuuza nyota huyo raia wa Misri wakati ni mchezaji mwenye kiwango kikubwa.

Kutokana na maswali hayo, mchambuzi wa soka, Jamie Carragher aeleza sababu haswa iliyomfanya kocha huyo raia wa Ureno kumuuza nyota huyo na kukmruhusu aondoke klabuni Chelsea.

"Ukizungumzia juu ya mabadiliko yake tusisahau kwamba amekuwa na maisha mazuri na bora katika soka lake. Ilikuwa ni Chelsea tu ndipo alishindwa kung'aa vizuri. Alishindwa kung'aa kwa vile alikosa muda mrefu wa kuonyesha alichonacho"

"Labda alikuwa akihisi huenda kocha Jose Mourinho alikuwa hana imani nae, ila ukichunguza ilikuwa ni ngumu kwake kuwa katika hadhi ya kocha yule, mara nyingi alikuwa anataka mtu anayejilinda kwanza kisha ndio ashambulie" alisema mchamuzi huyo.

Salah alicheza Chelsea kuanzia mwaka 2014 mpaka mwaka 2016 huku akiichezea michezo 13 na kuifungia magoli 2 na kwa sasa anaiongoza vyema klabu ya Liverpool.



No comments:

Post a Comment